Afrika ya Mashariki
Muhtasari wa masuala ya mazingira kusini mwa Afrika / From Wikipedia, the free encyclopedia
Afrika ya Mashariki ni sehemu ya bara la Afrika ambayo iko upande wa mashariki, ikipakana na Bahari ya Kihindi.
Kadiri ya Umoja wa Mataifa Afrika ya Mashariki ina nchi 18 zifuatazo:
- Burundi (mji mkuu Bujumbura)
- Djibouti (mji mkuu Jibuti (mji))
- Eritrea (mji mkuu Asmara)
- Ethiopia (mji mkuu Addis Abeba)
- Kenya (mji mkuu Nairobi)
- Komori (mji mkuu Moroni)
- Madagaska (mji mkuu Antananarivo)
- Malawi (mji mkuu Lilongwe)
- Morisi (mji mkuu Port Louis)
- Mozambique (mji mkuu Maputo
- Rwanda (mji mkuu Kigali)
- Zambia (mji mkuu Lusaka)
- Shelisheli (mji mkuu Victoria)
- Zimbabwe (mji mkuu Harare)
- Somalia (mji mkuu Mogadishu)
- Sudan Kusini (mji mkuu Juba)
- Tanzania (mji mkuu Dodoma)
- Uganda (mji mkuu Kampala)
- Mayotte na Réunion, zilizokuwa makoloni na sasa ni mikoa ya Ufaransa, zinahesabiwa pia katika orodha hii.
Hata hivyo:
- Malawi, Zambia na Zimbabwe wakati mwingine zinehesabiwa kuwa sehemu ya Afrika ya Kusini (zamani zilikuwa pamoja kama Rhodesia ya Kusini, Rhodesia ya Kaskazini na Unyasa katika Shirikisho la Afrika ya Kati)
- Komori, Morisi, Shelisheli, Mayotte na Réunion ni visiwa vidogo vya Bahari Hindi vinavyohesabiwa kuwa sehemu za Afrika ya Mashariki.