Kameruni, kirasmi Jamhuri ya Kameruni, ni jamhuri ya muungano katika Afrika ya Magharibi.

Ukweli wa haraka Jamhuri ya Kameruni, Mji mkuu ...
Jamhuri ya Kameruni
République du Cameroun (Kifaransa)
Republic of Cameroon (Kiingereza)
Thumb
Nembo
Kaulimbiu ya taifa:
Paix – Travail – Patrie (Kifaransa)
Peace – Work – Fatherland (Kiingereza)
"Amani – Kazi – Nchi"
Wimbo wa taifa: Chant de Ralliement
Thumb
Mahali pa Kamerun
Mji mkuuYaunde
3°52 N 11°31 E
Mji mkubwa nchiniDuala
04°03 N 09°41 E
Lugha rasmi
SerikaliJamhuri yenye mdikteta
  Rais
  Waziri Mkuu
Paul Biya
Joseph Dion Ngute
Eneo
  Eneo la jumlakm2 475 440[1]
  Maji (asilimia)0.57[1]
Idadi ya watu
  Kadirio la 202330 135 732[1]
Pato la taifaKadirio la 2023
  JumlaOngezeko USD bilioni 49.262[2]
  Kwa kila mtuOngezeko 1 721[2]
Pato halisi la taifaKadirio la 2023
  JumlaOngezeko USD bilioni 133.335[2]
  Kwa kila mtuOngezeko USD 4 660[2]
Maendeleo (2021)Imara 0.576[3] - wastani
SarafuFaranga ya CFA
Majira ya saaUTC+1
(Afrika Magharibi)
Upande wa magariKulia
Msimbo wa simu+237
Msimbo wa ISO 3166CM
Jina la kikoa.cm
Funga

Imepakana na Nijeria, Chadi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kongo, Gabon, Gine ya Ikweta na Ghuba ya Gine.

Lugha rasmi na lugha za taifa ni Kifaransa (kinachoongoza kwa zaidi ya asilimia 80) na Kiingereza.

Jiografia

Thumb
Mpare kwa mlima Kameruni
Makala kuu: Jiografia ya Kamerun
Thumb
Mlima Kamerun kutoka Tiko, Mkoa wa Kusini-Magharibi

Maeneo kiutawala

Makala kuu: Mikoa ya Kamerun na Wilaya za Kamerun

Kameruni imegawiwa katika mikoa (regions) 10 na wilaya (départements) 58.

Mikoa ni:


Ona pia: Orodha ya miji ya Kameruni

Historia

Historia ya awali

Katika karne za BK Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi walianza uenezi wao kutoka huko kwenda kutawala maeneo mengi ya Afrika ya Kati, Kusini mwa Afrika na Afrika Mashariki.

Wakati wa ukoloni

Kameruni ilikuwa koloni la Ujerumani hadi Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Baada ya Ujerumani kushindwa vita, nchi ikagawiwa kati ya Uingereza na Ufaransa chini ya mamlaka ya Shirikisho la Mataifa kama eneo la kudhaminiwa.

Tangu uhuru hadi leo

Mwaka wa 1960, Wafaransa waliacha Kameruni ikawa nchi huru. Wananchi wa Kameruni ya Kiingereza walipiga kura kuamua kama walitaka kuwa sehemu ya Nigeria au ya Kameruni. Kaskazini wengi walipendelea kukaa Nigeria, hivyo maeneo hayo sasa ni sehemu ya Nigeria. Wananchi wengi wa kusini waliamua wajiunge na Kameruni[4]. Kwa kusudi la kuheshimu tofauti za kiutamaduni kulikuwa na katiba mpya kwenye mwaka 1961 Shirikisho la Jamhuri ya Kameruni.

Tangu 1972 muundo wa nchi ulibadilishwa kuacha mfumo wa shirikisho na kuwa jamhuri ya muungano inayokazia zaidi matumizi ya lugha ya Kifaransa ingawa Kiingereza bado ni moja ya lugha rasmi. Jina la nchi pia likabadilishwa kuwa Jamhuri ya Muungano ya Kameruni mwaka wa 1972. Hapo sehemu ya Wakamerun wanaotumia lugha ya Kiingereza walijisikia kuwa wananyimwa haki zao.[5] Baadaye, mwaka wa 1984 jina likabadilishwa tena kuwa Jamhuri ya Kameruni (kwa Kifaransa République du Cameroun).

Tangu mwaka 2016 upinzani uliongezeka kati ya watu wa magharibi wanaotumia Kiingereza. Harakati hiyo ilijibiwa na serikali na polisi kwa ukali na hii umeleta kuanzishwa kwa wanamgambo wenye silaha wanaoshambulia polisi na jeshi la serikali kuu. Tangu mwaka 2017 wapinzani wamedai uhuru wa sehemu yenye lugha ya Kiingereza wakitangaza wameunda nchi mpya ya "Ambazonia". Serikali iliundwa inayokaa Nigeria; lakini kuna vikundi tofauti ambavyo wanapigana kati yao[6]. Nchi hii haitambuliwi kimataifa. Mwaka 2021 kulikuwa na majadiliano kuhusu amani kati kundi linalojiita serikali ya Ambazonia na serikali ya Kameruni[7], lakini makundi mengine yaliendelea na mapigano ya silaha[8].

Siasa

Thumb
Rais wa Kameruni Paul Biya (kulia)
Makala kuu: Siasa za Kamerun

Uchumi

Thumb
Majani chai inayotoka Kameruni
Makala kuu: Uchumi wa Cameroon

Watu

Thumb
Yaoundé, mji mkuu wa Kameruni (2003)
Thumb
Picha, kaskazini mwa Kameruni
Thumb
Ikulu ya sultani wa Bamun kwa Foumban, Mkoa wa Magharibi
Makala kuu: Watu wa Kamerun na Orodha ya lugha za Kamerun

Wakazi walikuwa 22,534,532 mwaka 2013, ambao wamegawanyika sawasawa kati ya wanaoishi mijini na wale wa vijijini.

Lugha rasmi ni Kifaransa pamoja na Kiingereza. Hata hivyo wakazi wanaongea pia lugha za makabila yao mengi.

Upande wa dini, 70% ni Wakristo (40% Wakatoliki na 30% Waprotestanti), 18% ni Waislamu, 3% ni wafuasi wa dini asilia za Kiafrika. 6% hawana dini yoyote.

Utamaduni

Thumb
Nyumba ya Njem
Thumb
Mwanamke wa Maka akienda shamba
Thumb
Familia ya Tikar, Kaskazini magharibi
Makala kuu: Utamaduni wa Kamerun, Muziki wa Kamerun, Mapishi ya Kamerun, na Waandishi wa Kamerun

Elimu

Makala kuu: Elimu Kamerun

Tazama pia

Marejeo

Viungo vya nje

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.