nchi katika Ulaya Kaskazini From Wikipedia, the free encyclopedia
Udeni (kwa Kideni: Kongeriget Danmark) ni ufalme wa Ulaya ya Kaskazini. Ni nchi ndogo kati ya nchi za Skandinavia.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: hakuna | |||||
Wimbo wa taifa: Der er et yndigt land (kitaifa); Kong Christian (kifalme) | |||||
Mji mkuu | Kopenhagen | ||||
Mji mkubwa nchini | Kopenhagen | ||||
Lugha rasmi | Kideni1 | ||||
Serikali Mfalme Waziri Mkuu |
Ufalme wa kikatiba Frederik X Mette Frederiksen | ||||
Kuungana kwa nchi {{{established_events}}} |
mnamo 980 BK | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
43,094 km² (ya 1341) 1.6%1 | ||||
Idadi ya watu - 2016 kadirio - 2006 sensa - Msongamano wa watu |
5,707,251 (ya 113) 5,450,661 132.96/km² (ya 783) | ||||
Fedha | Kroner (DKK ) | ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
CET3 (UTC+1) CEST3 (UTC+2) | ||||
Intaneti TLD | {{{cctld}}} | ||||
Kodi ya simu | +453 | ||||
1 Habari zote za Udeni bila Faroe na Grinilandi. |
Imepakana na Ujerumani upande wa kusini na kuzungukwa na maji pande tatu zilizobaki. Kaskazini kwake iko Norwei ng'ambo ya mlango wa bahari ya Skagerak, mashariki iko Uswidi ng'ambo ya Kattegat na Oresund. Bahari ya Kaskazini iko upande wa magharibi, Baltiki inaanza kwenye visiwa vikuu vya Udeni.
Greenland na visiwa vya Faroe ni sehemu ya ufalme wa Udeni lakini zinajitawala.
Udeni ina eneo la km² 43.000. Theluthi ya eneo hili ni kwenye visiwa 443 vya Udeni ambavyo 76 tu kati yake vinakaliwa na watu.
Visiwa vikubwa ni Funen (Fyn), Zealand (Sjælland) na Bornholm (Bornholm).
Rasi ya Jutland ni sehemu kubwa ya eneo. Jutland ni Udeni bara. Ina urefu wa km 300 kuelekea kaskazini kutoka mpaka wa Ujerumani hadi ncha yake kwa Skagen.
Kwa jumla Udeni iko tambarare. Mwinuko wa juu una kimo wa m 170 pekee juu ya UB.
Kumbuka kwamba orodha hii inahusu Udeni tu kama nchi, si Visiwa vya Faroe na Greenland.[1][2] Mlima mrefu wa ufalme mzima ni Gunnbjørn, Greenland, m 3,700 juu ya UB.
No | Mwinuko | Sehemu ya Nchi | Kimo |
---|---|---|---|
1. | Møllehøj | Skanderborg manisipaa | 170,86 d |
2. | Yding Skovhøj | Horsens manisipaa | 170,77 d |
3. | Ejer Bavnehøj | 170,35 d | |
4. | Lindbjerg | 170,08 d | |
5. | Basi Margretelyst | 169,78 d | |
6. | Vistofte | 169,44 d | |
Mpaka mwaka 1847 Himmelbjerget, Skanderborgs, m 147 ilifikiriwa kuwa mwinuko mkubwa wa Udeni.
Wakazi wa kwanza waliojulikana katika historia kwa jina ni makabila ya Wakimbri na Wateutonia waliohamia hadi Ulaya ya kusini wakati wa njaa mnamo mwaka 113 KK.
Katika karne ya 8 hadi karne ya 11 BK majambazi wa baharini kutoka Udeni na Norway waliogopwa kote Ulaya kwa jina la "Waviking". Walivamia pia Uingereza mara kwa mara na kujenga makao huko. Tangu mwaka 793 walitawala eneo la Danelag (au: Danelaw) kaskazini na kaskazini-mashariki mwa Uingereza wa leo.
Katika karne ya 8 na karne ya 10 maeneo madogo yaliunganishwa. Wafalme wa kwanza wanaojulikana kutawala Udeni yote walikuwa Garm Mzee na Harald Jino Buluu (mnamo mwaka 980). Harald alikuwa mfalme wa kwanza wa kupokea Ukristo wa Kanisa Katoliki.
Udeni ikawa nchi yenye nguvu katika Skandinavia na kwenye pwani za Baltiki.
Kuanzia 1397 hadi 1521 nchi zote za Skandinavia ziliunganishwa katika maungano ya kifalme chini ya wafalme wa Udeni ilhali kila nchi ilijitawala katika mambo ya ndani.
Baada ya Uswidi kujitenga na umoja huo, Norway iliendela kuwa chini ya Udeni hadi mwaka 1814.
Mwaka 1537 Udeni ilijiunga na Matengenezo ya Kiprotestanti na Kanisa la Kilutheri likawa dini rasmi nchini hadi leo, ikifuatwa na 76.9% za wakazi. Udeni ilikuwa kati ya nchi muhimu sana ya Ulutheri, lakini leo 3% tu wanashiriki ibada ya Jumapili.
Baada ya vita za Napoleoni Udeni iliondolewa utawala wa Norway iliyounganishwa na Uswidi mwaka 1814. Lakini makoloni ya Greenland, Iceland, Faroe na visiwa vya Karibi zilibaki chini yake.
Karne ya 19 ilileta fitina na Ujerumani juu ya utawala wa Schleswig na Holstein. Baada ya vita ya 1864 Udeni ilipaswa kuacha majimbo hayo mawili kwa Ujerumani.
Udeni haikushiriki katika Vita Kuu ya Dunia ya Kwanza lakini ilirudishwa sehemu ya kaskazini ya jimbo la Schleswig.
Wakati wa Vita Kuu ya Dunia ya Pili Udeni ilivamiwa na Ujerumani mwaka 1940 hadi 1945. Wakati wa vita Iceland iliamua kutangaza uhuru wake.
Mwaka 1948 mara baada ya vita visiwa vya Faroe vilipewa madaraka ya kujitawala lakini vilibaki ndani ya umoja na Udeni. Koloni la Greenland lilipewa madaraka hayo mwaka 1979.
Udeni ikawa kati ya nchi zilizounda UM na pia NATO.
Mwaka 1973 ikajiunga na Jumuiya ya Ulaya (sasa: Umoja wa Ulaya), lakini imekataa kutumia euro badala ya krona.
Kutokana na uzazi mdogo, miaka ya mwisho uhamiaji umeongezeka, hivi 12.3% wana asili ya kigeni (yaani hata mzazi wao mmoja ni raia na mzaliwa wa Udeni).
Mnamo Januari 2017, wakazi walikuwa 5,748,769. Kati yao, Wadeni asili ni 88,67%. Wengine ni wahamiaji (kutoka Poland, Uturuki, Ujerumani, Iraq, Romania, Syria, Somalia, Iran, Afghanistan n.k.) au wamezaliwa na mhamiaji walau mmoja.
Lugha ya nchi ni Kideni, jamii ya Kijerumani, na 86% za wakazi huongea vizuri Kiingereza kama lugha ya pili.
Upande wa dini, wengi ni Wakristo, lakini 3% tu wanashiriki ibada ya Jumapili na 19% tu wanaona dini ni muhimu maishani. Dini rasmi ni Kanisa la Udeni (la Kilutheri; 75.9%). Wakatoliki hawafikii 1%. Kutokana na uhamiaji, Waislamu ni 3.7%.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.