From Wikipedia, the free encyclopedia
Greenland (kwa Kiswahili Grinilandi pia; kwa Kikalaallisut: Kalaallit Nunaat = Nchi ya Wagreenland) ni nchi ya kujitawala chini ya ufalme wa Denmark lakini haihesabiwi kuwa sehemu ya Denmark yenyewe.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: | |||||
Wimbo wa taifa: Nunarput utoqqarsuanngoravit Nuna asiilasooq | |||||
Mji mkuu | Nuuk (Godthåb) | ||||
Mji mkubwa nchini | Nuuk (Godthåb) | ||||
Lugha rasmi | {{{official_languages}}} | ||||
Serikali | Demokrasia (serikali ya kibunge ndani ya ufalme wa kikatiba) Frederik X wa Denmark Múte Bourup Egede 2021 | ||||
Eneo la kujitawala Kujitawala |
1979 na zaidi 2009 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
2,166,086 km² (ya 12) 83.1a | ||||
Idadi ya watu - Machi 2022 kadirio - Msongamano wa watu |
56,583 (ya 210) 0.028/km² (ya 244) | ||||
Fedha | Krone ya Denmark (DKK ) | ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC0 to -4) (UTC) | ||||
Intaneti TLD | .gl | ||||
Kodi ya simu | +299
- | ||||
a As of 2000: 410,449 km² (158,433 sq. miles) ice-free; 1,755,637 km² (677,676 sq. miles) ice-covered. b 2001 estimate. |
Eneo la Greenland ni kubwa, lakini idadi ya wakazi ni ndogo sana kwa sababu sehemu kubwa ya nchi (75%) imefunikwa na ganda nene la barafu.
Jina la Kiswahili limetokana na lile la Kiingereza "Greenland", ambalo ni tafsiri ya jina la Kidenmark "Grønland", linalomaanisha "nchi yenye rangi ya majani mabichi".
Jina hilo Greenland lilitungwa miaka 1000 iliyopita, kwa sababu wakati ule hali ya hewa duniani ilikuwa na joto zaidi, na hapakuwa na barafu nyingi kama leo.
Kijiografia Greenland, kisiwa kikubwa kuliko vyote duniani, ni sehemu ya bamba la Amerika ya Kaskazini lakini kihistoria na kisiasa kwa karne kadhaa imekuwa na uhusiano wa karibu na Skandinavia (Ulaya ya Kaskazini).
Mlima wa juu wa Greenland ni Mlima Gunnbjørn (m 3,694 juu ya UB) katika Watkins Range.
Wananchi wengi (89.5%) ni wakazi asilia wenye asili ya Asia, ingawa wengi wao wana pia damu ya Kizungu kwa asilimia 25. Lugha yao ndiyo lugha rasmi pekee tangu mwaka 2009. 8.6% ni Wazungu wenye asili ya Skandinavia na wanaongea Kidenmark ambacho kinaendelea kutumiwa na wote katika nafasi kadhaa. Wakazi wengi wanaweza kuongea lugha zote mbili.
Upande wa dini, walio wengi ni Wakristo (96.1%), hasa Walutheri (85%).
Greenland inaongoza duniani kwa asilimia ya watu wanaojiua, pamoja na kuwa na idadi kubwa ya walevi.
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
|
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.