Remove ads

Uzazi ni mchakato wa kibiolojia ambao kiumbe hai kipya kinapatikana kutokana na kingine au vingine.

Thumb
Upatikanaji wa mimea mipya pembeni mwa jani la Miracle Leaf plant, Kalanchoe pinnata.

Uwezo wa kuzaa ni kati ya sifa kuu zinazotambulisha uwepo wa uhai; kila kiumbe hai kilichopo duniani kimetokana na uzazi. Inakadiriwa kwamba kiumbe hai kilichozaa vile vyote vilivyopo leo kiliishi miaka 3,500,000,000 hivi iliyopita.

Njia za uzazi

Kuna njia mbili za uzazi: ile isiyotegemea jinsia, na ile inayoitegemea.

Katika uzazi usiotegemea jinsia, kiumbe hai huzaa peke yake. Unatokea hasa katika viumbe vinavyoundwa na seli moja tu, lakini si hivyo tu. Kwa njia hiyo kiumbe hai kipya ni sawa na mzazi kwa sababu kimerithi jenomu ileile.

Wanabiolojia hawajaelewa ilikuwaje kwamba katika maendeleo ya uhai (mageuko ya spishi) uzazi huo umeacha nafasi kwa ule wa kijinsia unaodai wahusika wawe wawili, na hivyo kupunguza uzazi kwa asilimia 50.[1][2]

Uzazi wa kijinsia huwa unadai mchango wa wazazi wawili ambao kila mmojawao anakichangia kiumbe hai kipya kwa asilimia 50 za chembeuzi zake.

Remove ads

Uzazi wa binadamu

Binadamu akiwemo kati ya mamalia anazaa kwa namna inayofanana hasa na ile ya wanyama hao. Hata hivyo, akiwa na akili na utashi, anatakiwa kuratibu silika yake kuhusu uzazi ili uendane na uwajibikaji.

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Marejeo mengine

Remove ads

Viungo vya nje

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.

Remove ads