From Wikipedia, the free encyclopedia
Senegal (pia Senegali) ni nchi ya Afrika ya Magharibi iliyopo upande wa kusini wa mto Senegal.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Un Peuple, Un But, Une Foi (Kifaransa: Taifa moja, Lengo moja, Imani moja) | |||||
Wimbo wa taifa: Pincez Tous vos Koras, Frappez les Balafons' | |||||
Mji mkuu | Dakar | ||||
Mji mkubwa nchini | Dakar | ||||
Lugha rasmi | Kifaransa | ||||
Serikali Rais Waziri Mkuu |
Jamhuri Macky Sall Sidiki Kaba | ||||
Uhuru kutoka Ufaransa |
20 Juni 1960 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
196,712 km² (ya 87) {{{percent_water}}} | ||||
Idadi ya watu - 2023 kadirio - 2015 sensa - Msongamano wa watu |
18,384,660 (ya 66) 13,508,715 93.3/km² (134) | ||||
Fedha | CFA Franc ({{{currency_code}}} ) | ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
UTC (UTC+0) (UTC) | ||||
Intaneti TLD | .sn | ||||
Kodi ya simu | +221
- |
Imepakana na Mauritania upande wa kaskazini, Mali upande wa mashariki, Guinea na Guinea-Bisau kusini na Bahari Atlantiki upande wa magharibi.
Nchi ya Gambia inazungukwa na eneo la Senegal isipokuwa upande wa bahari.
Visiwa vya Cabo Verde viko km 560 mbele ya pwani ya Senegal.
Senegal ni nchi inayogusana na kanda ya Sahel na pia kanda ya Tropiki.
Uso wa nchi ni hasa tambarare zinazopanda juu polepole kuelekea kusini mashariki. Sehemu nyingine zinafikia mita 580 juu ya UB. Kusini kabisa iko kasoko kubwa la Velingara.
Hali ya hewa ni ya kitropiki. Majira ya mvua ni hasa miezi ya Mei hadi Novemba.
Nchi imegawanyika katika mikoa 14 iliyogawanyika tena katika wilaya 45.
Miji mikubwa ni Dakar (wakazi 2 476 400), Pikine (wakazi 874 062), Thiès (wakazi 252 320), Saint-Louis (wakazi 176 000), Kaolack (wakazi 172 305), Ziguinchor (wakazi 159,788), Tiebo (wakazi 100 289). Karibu nusu ya watu huishi mijini.
Kwa wakati na kiasi tofauti eneo la Senegal lilikuwa sehemu ya Dola la Ghana, ya Dola la Mali na hatimaye ya Dola la Songhai
Kuna wakazi milioni 13.5 na idadi kubwa ni wa chini ya umri wa miaka 20. Wameongezeka sana, mnamo mwaka 1985 idadi ilikuwa milioni 5 tu.
Kikundi kikubwa nchini ni Wawolof (43%), wengine ni Wafula wakiwa pamoja na Watukulur (24%), halafu Waserer (14.7%), Wadiola (4%),Wamandinka (3%), Wasoninke.
Kwa ujumla kuna lugha 37 nchini Senegal. Kiwolofu kinazidi kuenea, lakini mpaka sasa lugha rasmi ni Kifaransa. Shuleni kinatumika pia Kireno, hasa kusini.
Theluthi mbili ya wakazi hawajui kusoma.
Senegal ni nchi isiyo na dini rasmi. Wakazi wengi sana (94%) ni Waislamu (hasa Wasunni); Wakristo (hasa Wakatoliki) ni takriban 5%.
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Senegal kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.