Nyangumi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Nyangumi ni wanyama wa bahari, na pengine wa maji matamu, katika oda Cetacea wanaofanana na samaki, lakini ni mamalia: kwa hivyo hawatagi mayai kama samaki bali huzaa watoto kama mamalia wote na huwanyonyesha.
Nyangumi | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Makundi 3:
| ||||||||||||||
Pamoja na nguva, wanyama hawa ni mamalia pekee wanaoishi kwenye maji tu.
Oda yao ina spishi 80 hivi. Spishi ndogo huitwa pomboo kwa kawaida na spishi kadhaa za pomboo huishi kwenye maji matamu ya mito mikubwa kama Ganges au Amazonas.
Mwili wote unalingana na maisha ya majini. Nyangumi wanaotupwa kwenye nchi kavu wanakufa haraka: wanakauka, uzito wa mwili unagandamiza mapafu kwa sababu wanakosa ueleaji wa maji.
Hata hivyo muundo wa mwili ni sawa na mamalia wengine:
- wanapumua kwa kutumia mapafu; kutegemeana na spishi zinaweza kuzama na kukaa chini ya maji kuanzia dakika kadhaa hadi masaa mawili.
- Huwa na moyo wenye vyumba vinne unaoweza kusambaza oksijeni mwilini mwote.
- Nyangumi huwa na damu moto yaani wanaweza kutunza halijoto ya wastani mwilini, tofauti na samaki wanaobadilika halijoto ya mwili kulingana na halijoto ya mazingira.
- Wanazaa watoto waliokamilika tayari na kuwanyonyesha maziwa yenye mafuta mengi kwa kutumia viwele vyao. Mimba hukua mwilini mwa mama hadi kuwa mnyama kamili jinsi ilivyo kwa mamalia wengi.
Spishi nyingi za nyangumi ni kubwa sana. Nyangumi buluu (Blue whale) anaweza kufikia uzito wa tani 200 na urefu wa mita 33. Nyangumi wadogo ni hasa familia ya pomboo ambao wale wadogo wanafikia urefu wa mita na nusu tu.
Mara nyingi spishi za nyangumi zinatofautishwa kutokana na meno yao:
- wale wanaowinda samaki au wanyama wakubwa wengine wa bahari wana meno ya kawaida.
- wale wanaokula planktoni (viumbe hai vidogo sana baharini) hawana meno, bali mifupa ya kinywani ambao si mifupa ya kweli, ila inaundwa na kitu kinachofanana na kucha za vidole. Mifupa hiyo inakaa kama meno ya chanuo na inafanya kazi ya filta; nyangumi huyo anafungua mdomo na kujaza nafasi maji pamoja na yote yaliyomo kama uduvi wadogo sana; ulimi unasukuma maji kupitia chanua ya mifupa ya kinywani na windo unabaki ndani kama chakula.
Nyangumi ni jina la jumla la mamalia wa majini wa oda ya Cetacea. Neno nyangumi wakati fulani humaanisha wanyama wote wa oda ya Cetacea, lakini katika lugha ya kawaida huwaacha wanyama wa familia ya Delphinoidea, kama vile pomboo.
Spishi ndogo hizi huwa ndani ya oda ndogo ya Odontoceti (nyangumi wenye meno), ambayo hujumuisha nyangumi kadhaa.
Oda nyingine ndogo ya Cetacea ni Mysticeti, ambayo hujumuisha nyangumi wa bluu, ambaye ndiyo mnyama mkubwa kuliko wote aliyeripotiwa kuishi, nyangumi mwenye nundu, na wanyama wengine wanaokula kutoka kwenye maji ya baharini kutumia michirizi mirefu iliyopo badala ya meno, ambayo ndiyo walikopatia jina lao.