![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/f/fc/Illu_mouth_%2528Kiswahili%2529.jpg/640px-Illu_mouth_%2528Kiswahili%2529.jpg&w=640&q=50)
Kinywa
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kinywa au mdomo ni uwazi ndani ya kichwa mwenye shughuli tofauti kwa binadamu na wanyama wengi wenye uti wa mgongo.
- ni mahali pa kuingiza chakula mwilini hivyo ni chanzo cha mfumo wa mmeng'enyo wa chakula
- ni nafasi ya kuingiza hewa mwilini hivyo pamoja na pua ni chanzo cha mfumo wa upumuo
- ni mahali pa kutokea kwa sauti ambako sauti inayotengenezwa kooni inapokea umbo lake kwa msaada wa ulimi na midomo hivyo ni sehemu muhimu ya uwezo wetu wa kuwasiliana na wengine.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/f/fc/Illu_mouth_%28Kiswahili%29.jpg/320px-Illu_mouth_%28Kiswahili%29.jpg)
Kinapatikana kwa karibu wanyama wote wenye seli nyingi lakini kwa wanyama sahili kazi yake ni kuingiza chakula pekee.
Sehemu za kinywa cha binadamu ni pamoja na: meno, ulimi na fizi.