From Wikipedia, the free encyclopedia
Uti wa mgongo ni nguzo ya mifupa ambayo ni kiini cha kiunzi cha mifupa katika miili ya vetebrata kama binadamu, mamalia wote na pia wanyama wengine wengi kama samaki, reptilia na ndege.
Nguzo hii ya uti wa mgongo inashikamanisha mifupa yote kwa pamoja kuanzia fuvu na mabavu hadi mifupa ya chini inayokutana katika fupanyonga.
Pamoja na kuwa kiini cha kiunzi cha mifupa, uti wa mgongo huwa na kazi ya pili muhimu: inatunza ndani yake neva za ugwemgongo zinazofikisha amri za ubongo mwilini mwote. Neva za ugwembongo ni nyeti sana; hivyo uharibifu kwenye uti wa mgongo unaoathiri neva hizo kiasi unaweza kusababisha maumivu makali au hata ulemavu kama neva zinakatika na sehemu za mwili hazipokei tena amri kutoka ubongo.
Uti wa mgongo unafanywa na pingili au vetebra 33-35, kutegemeana na umri wa mtu; tofauti hutokea kwenye sehemu ya kifandugu. Pingili 24 za juu zinatenganishwa na visahani vya vetebra. Huangaliwa na matibabu kuwa sehemu kuu tano:
Makala hii kuhusu mambo ya anatomia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Uti wa mgongo kama matumizi yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.