Mkoa wa Tanzania From Wikipedia, the free encyclopedia
Mkoa wa Mwanza ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania, wenye postikodi namba 33000.
Mkoa wa Mwanza |
|
Mahali pa Mkoa wa Mwanza katika Tanzania | |
Majiranukta: 2°45′S 32°45′E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Wilaya | 8 |
Mji mkuu | Mwanza |
Serikali | |
- Mkuu wa Mkoa | Abas Kandoro |
Eneo | |
- Jumla | 19,592 km² |
Idadi ya wakazi (2022) | |
- Wakazi kwa ujumla | 3,699,872 |
Tovuti: http://www.mwanza.go.tz/ |
Umepakana na Geita upande wa magharibi, Shinyanga na Simiyu upande wa kusini na Mara upande wa mashariki. Ziwa la Viktoria Nyanza liko kaskazini.
Makao makuu ya mkoa yapo Mwanza mjini.
Mkoa una wakazi 3,699,872 kadiri ya sensa ya mwaka 2022 [1].
Kabla ya kumegwa na kuzaa mkoa mpya wa Geita, mkoa wa Mwanza ulikuwa na wakazi 2,942,148 (sensa ya mwaka 2002) katika wilaya 8 ukiwa na eneo la 19,592 km2.
Wilaya ndizo Ukerewe, Magu, Sengerema, Buchosa, Misungwi, Kwimba, Nyamagana na Ilemela. Jiji la Mwanza ndani yake lina wilaya za Nyamagana na Ilemela.
Ramani (kabla ya 2012) | Wilaya au manisipaa | Wakazi (2022) | Tarafa | Kata | Kijiji | Eneo km² |
---|---|---|---|---|---|---|
Wilaya ya Buchosa | 413,110 | |||||
Wilaya ya Ilemela | 509,687 | |||||
Wilaya ya Kwimba | 480,025 | |||||
Wilaya ya Magu | 421,119 | |||||
Wilaya ya Misungwi | 467,867 | |||||
Wilaya ya Nyamagana | 594,834 | |||||
Wilaya ya Sengerema | 425,415 | |||||
Wilaya ya Ukerewe | 387,815 | |||||
Jumla | 3,699,872 | |||||
Marejeo: Mkoa wa Mwanza |
Makabila makubwa ya Mwanza ndio Wasukuma na Wazinza upande wa bara, halafu Wakerewe na Wakara visiwani.
Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.