Remove ads

Msimbo wa posta (pia postikodi) [1] (ing. post code, ZIP au PIN) ni ufutanao wa tarakimu au herufi unaotaja eneo ambako barua inatakiwa kufikishwa.

Thumb
Stempu ya Kirusi mnamo mwaka 1977 inayotangaza matumizi ya misimbo ya posta
Thumb
Sehemu za msimbo wa posta wa Kanada (herufi + tarakimu)

Siku hizi posta za nchi nyingi za dunia hutumia misimbo hii. Kusudi lake ni kurahisisha kazi ya kuchambua na kutenganisha barua zinazopokelewa kufuatana na mahali zinapotumwa. Si lazima tena mfanyakazi wa posta ajue mahali pengi inatosha kugawa barua kufuatana na misimbo iliyoandikwa kwenye bahasha. Kwa hiyo misimbo hupangwa kufuatana na utaratibu wa kugawa na kusafirisha barua.

Kwa matumizi ya teknolojia ya kisasa kuna pia mashine zinazochambua barua zikitambua namba kwenye bahasha.

Nchi zilizo nyingi hutumia tarakimu pekee katika msimbo wa posta. Nchi zifuatazo huunganisha herufi na tarakimu: Argentina, Bermuda, Brunei, Kanada, Jamaika, Malta, Uholanzi, Ufalme wa Maungano (=Uingereza) na Venezuela.

Katika Kenya na Tanzania kuna mfumo wa msimbo wa posta mwenye tarakimu tano. (Tazama pia Mfumo wa Msimbo wa Posta Tanzania na Mfumo wa Msimbo wa Posta Kenya)

Kwa mfano barua kwa mteja huko Nairobi-Westlands awe na msimbo wa posta 00800, halafu jina na namba ya sanduku la posta; kwa mteja huko Ololulunga katika Bonde la Ufa msimbo ni 20503.

Vivyo hivyo katika Tanzania barua kwenda Kashaulili huko Mpanda katika Mkoa wa Katavi iwe na msimbo 50106; mfanyakazi hahitaji kukumbuka jina na kata hii inatosha akiona msimbo uananza kwa tarakimu 5 ataweka bahasha katika kikapu cha Katavi.  

Remove ads

Marejeo

Tazama pia

Viungo vya Nje

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.

Remove ads