Mkoa wa Manyara
From Wikipedia, the free encyclopedia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mkoa wa Manyara ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 27000. Umepakana na mikoa ya Arusha na Kilimanjaro upande wa kaskazini, Mkoa wa Tanga upande wa mashariki, Mkoa wa Dodoma upande wa kusini na mikoa ya Singida na Shinyanga upande wa magharibi.
Mkoa wa Manyara umetengwa na Mkoa wa Arusha mwaka 2002 kwa azimio la rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ukiwa na eneo la km² 46,359.
Babati ndiyo makao makuu ya mkoa.
Jumla ya wakazi mkoani ilikuwa 1,892,502 katika sensa ya mwaka 2022 [1].
Idadi hiyo imepatikana katika wilaya 7 zifuatazo (katika mabano idadi ya wakazi mwaka 2022): Babati Vijijini (375,200), Babati Mjini (129,572), Hanang (367,391), Mbulu Vijijini (238,272), Mbulu Mjini (138.593), Simanjiro (291,169) na Kiteto (352,305).
Sensa zinaonyesha kwamba ni kati ya mikoa ya Tanzania yenye ongezeko kubwa la wakazi. Pia ni kati ya mikoa yenye maambukizi machache zaidi ya Ukimwi.
Wenyeji wa mkoa huu ni pamoja na Wairaqw, Wamasai, Wambugwe, Wagorowa na Wabarbaig wakijihusisha na shughuli za kilimo na ufugaji kama njia ya kuingiza kipato chao cha kila siku.
Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi 7 yafuatayo:
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.