Ludoviko wa Toulouse
From Wikipedia, the free encyclopedia
Ludoviko wa Toulouse (Brignoles, Provence, Ufaransa, Februari 1274 - Toulouse 19 Agosti 1297) alikuwa mwana wa mfalme wa Napoli Charles II wa Anjou, mdogo wake Ludoviko IX, lakini akitamani ufukara wa Kiinjili kuliko sifa na heshima za kidunia, alikataa haki ya kumrithi akawa mtawa wa Ndugu Wadogo na askofu wa Kanisa Katoliki mjini Toulouse[1].
Akiwa kijana kwa umri lakini mkomavu katika maadili alifariki mapema kutokana na afya wake dhaifu[2].
Alitangazwa na Papa Yohane XXII kuwa mtakatifu tarehe 7 Aprili 1317.