Papa Yohane XXII
From Wikipedia, the free encyclopedia
Papa Yohane XXII (takriban 1249 – 4 Desemba 1334) alikuwa Papa kuanzia mwaka 1316 hadi kifo chake. Alichaguliwa tarehe 7 Agosti 1316, na kuvishwa taji tarehe 5 Septemba mwaka uleule katika mji wa Lyon[1]. Alitokea Cahors, Ufaransa[2].
Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Jacques Duèse.
Alimfuata Papa Klementi V akafuatwa na Papa Benedikto XII.