Fedha
From Wikipedia, the free encyclopedia
Fedha kwa maana ya malipo au sarafu angalia makala ya pesa
Fedha (kutoka Kiarabu فضة fiddtan) ni elementi na metali yenye kifupi cha Ag (kutoka Kilatini: argentum) na namba atomia 47 katika mfumo radidia. Uzani atomia ni 107.86. Fedha huyeyuka kwa 1234.93 K (961.78°C) na kuchemka kwa 2435 K (2162°C).
Kiasili yatokea kama metali nyeupenyeupe na laini au kama mchanganyiko katika madini. Kati ya metali zote fedha ni wayaikaji na inapitisha vizuri umeme.