Kuku-mwamba
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kuku-mwamba ni ndege wakubwa kiasi wa jenasi Picathartes, jenasi pekee ya familia Picathartidae. Wanatokea misitu ya Afrika kusini kwa Sahara. Kuku-mwamba wana domo kubwa kama lile la kunguru na kichwa bila manyoya chenye rangi kali (nyeusi na njano au nyekundu). Pia wana rangi ya nyeusi au kijivucheusi juu na nyeupe chini. Shingo yao ni nyeupe au ina rangi ya kijivu. Hula wadudu, kama bungo, mchwa na sisimizi, pia majongoo, tandu, nyungunyungu, konokono na hata vyura na mijusi. Hulijenga tago lao kwa matope chini ya mwamba. Jike huyataga mayai mawili.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Kuku-mwamba | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kuku-mwamba shingo-nyeupe (Picathartes gymnocephalus) | ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Spishi 2:
| ||||||||||||||||
Msambazo wa kuku-mwamba (pinki=P. gymnocephalus; buluu=P. oreas) | ||||||||||||||||
Funga