Tandu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Tandu ni aina za arithropodi wembamba na warefu katika ngeli Chilopoda ya nusufaila Myriapoda wenye miguu mingi. Wanafanana kijuujuu na majongoo lakini hawa huenda polepole na hula dutu ya viumbehai, viani na kuvu. Tandu huenda mbio na hula wanyama wengine (invertebrati na vertebrati). Hata kama tandu huitwa centipedes (miguu mia) kwa Kiingereza na majongoo huitwa millipedes (miguu elfu), kwa ukweli wana kwa kadiri nambari sawa ya miguu: tandu wana miguu 16 hadi 300 na majongoo 36 hadi 750.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Tandu | ||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Tandu kichwa-chekundu | ||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||
| ||||||||
Ngazi za chini | ||||||||
Oda na familia:
Oda Lithobiomorpha
Oda Craterostigmomorpha
Oda Scolopendromorpha
Oda Geophilomorpha
| ||||||||
Funga