Jongoo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Majongoo ni aina za arithropodi wembamba na warefu katika ngeli Diplopoda ya nusufaila Myriapoda wenye miguu mingi. Wanafanana kijuujuu na tandu lakini hawa huenda mbio na hula wanyama wengine (invertebrati na vertebrati). Majongoo huenda polepole na hula dutu ya viumbehai, viani na kuvu.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Jongoo | ||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Majongoo panda wakijamiiana | ||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||
| ||||||||
Ngazi za chini | ||||||||
Nusungeli:
| ||||||||
Funga
Hata kama kwa Kiingereza majongoo huitwa millipedes (miguu elfu) na tandu huitwa centipedes (miguu mia), kwa ukweli wana idadi karibu sawa ya miguu: tandu wana miguu 16 hadi 300 na majongoo 36 hadi 750.