Konokono
From Wikipedia, the free encyclopedia
Konokono (pia koa lakini kwa kweli ni kombe la konokono) ni wanyama wa ngeli ya Gastropoda katika faila Mollusca. Neno konokono linatumika kujumuisha wale wa nchi kavu, wa maji baridi na wa bahari. Spishi nyingi zina koa lililojiviringisha na kukua katika hatua. Spishi nyingine zinakosa koa (au zinalo dogo sana) na huitwa konokono uchi.
Konokono | ||||||
---|---|---|---|---|---|---|
Helix pomatia, spishi ya konokono wa nchi kavu | ||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||
| ||||||
Ngazi za chini | ||||||
Oda 8:
| ||||||
Konokono hupatikana maeneo mengi kama vile miferejini, jangwani, hata kwenye vina virefu baharini. Ingawa watu wengi wanaufahamu na konokono wanaopatikana nchi kavu tu, hawa wa ardhini ni kidogo mno. Konokono wa majini ndio wengi sana na huchangia kiasi kikubwa cha spishi ya konokono na wana aina nyingi sana na hata maumbo ya kibailojia makubwa zaidi. Konokono wengine wengi kiasi pia hupatikana kwenye maji baridi. Konokono wengi hula majani, japo baadhi yao hula majani na nyama, na wengine huwinda na kula nyama tu.
Konokono wanaopumua kwa kutumia mapafu huwekwa kwenye kundi la Pulmonata, huku wale wenye yavuyavu huuunda kundi la paraphyletic group; kwa maneno mengine konokono wenye yavuyavu wameanishwa kwenye makundi yasiyo husianiana sana. Konokono wenye mapafu na wale wenye yavuyavu kwa nyakati nyingi za mabadiliko wa mfumo wa miamba imepelekea hata baadhi ya konokono wenye mapafu kuishi baharini na hata wale wenye yavuyavu nao kuishi nchi kavu Konokono wana maumbile maelfu yafananayo na meno. Meno haya maelfu madogo yanapatikana kwenye ulimi na hufanya kazi kama tupa na kusaga chakula kwenye vipande vidogo. Ulimi wao huitwa radula.