From Wikipedia, the free encyclopedia
Kanisa Katoliki la Armenia (kwa Kiarmenia Հայ Կաթողիկէ Եկեղեցի Hay Kat’oġikē Ekeġec’i) ni madhehebu ya Kanisa Katoliki yanayofuata mapokeo ya Kanisa la Armenia katika ushirika kamili na Papa wa Roma.
Ushirika huo ulidhoofika baada ya Mtaguso wa Kalsedonia (451), hasa kutokana na ugumu wa mawasiliano. Lakini haukuisha kabisa, na kwa nyakati mbalimbali uliweza kuimarishwa tena, hasa kuanzia 1195.
Kanisa hilo linatumia liturujia ya Armenia inayofuata mapokeo ya Gregori Mletamwanga, aliyeingiza taifa lote la Armenia katika Ukristo.
Mkuu wake anaitwa Patriarki wa Kilikia wa Waarmenia na kwa sasa ni Nerses Bedros XIX Tarmouni.
Makao makuu huko Bzoummar (Lebanoni, lakini waamini wengi wanaishi Armenia na katika nchi za kandokando. Wengine wanaishi sehemu nyingi duniani. Jumla wako 539,806 (2008).
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kanisa Katoliki la Armenia kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.