From Wikipedia, the free encyclopedia
Gregori Mletamwanga (kwa Kiarmenia Գրիգոր Լուսաւորիչ, Grigor Lusavorich, 257 hivi - 331 hivi) ndiye mwanzilishi na kiongozi wa kwanza wa Kanisa la Kitume la Armenia kwa kuongoa nchi nzima ya Armenia kutoka Upagani kuingia Ukristo mwaka 301. Hivyo Armenia ikawa taifa la kwanza kufanya dini hiyo kuwa dini yake rasmi.
Kisha kupata hivyo sifa ya kuwa Mtume wa Waarmenia kwa juhudi kubwa sana, alikwenda kuishi upwekeni yanapokutana matawimto mawili yanayounda mto Eufrate, akaishi huko hadi kifo chake[1].
Tangu kale anaheshimiwa na madhehebu mbalimbali ya Ukristo kama mtakatifu.
Sikukuu yake inaadhimishwa na Waarmenia tarehe 9 Juni, lakini na Wakristo wengine tarehe 30 Septemba[2].
Gregori alikuwa mtoto[3] wa watu wa koo bora za Armenia na Parthia[4] Anak Mparthia[5][6][7] na Okohe.
Anak alishutumiwa kwamba alimuua mfalme Khosrov II akauawa. Gregori alinusurika na kupelekwa Caesarea huko Kapadokia alipolelewa na Phirmilianos (Euthalius) kama Mkristo safi.
Baadaye Gregori alimuoa Miriam, binti wa mtawala wa Kiarmenia wa Kapadokia, wakapata watoto wawili, ambao pia wanaheshimiwa kama watakatifu: Vrtanes na Aristaces. Vrtanes aliendeleza ukoo, kumbe Aristaces akawa mwandamizi wa baba yake alipofariki. Hapo katikati Miriam na Gregori walitengana ili mume aweze kuingia umonaki, halafu Gregori alihama Kapadokia na kurudi Armenia ili kuiinjilisha kama fidia ya makosa ya baba yake.
Wakati huo alitawala Tiridates III, mwana wa Khosrov II. Huyo aliagiza Gregori afungwe miaka 12 au 14 ndani ya kisima karibu na Artashat. Alitolewa mwaka 297 hivi ili amponye Tiridates III, aliyechanganyikiwa kabisa baada ya kusalitiwa na kaisari wa Dola la Roma Diocletian aliyevamia na kuteka maeneo mengi ya magharibi mwa. Armenia Kubwa.
Mwaka 301 Gregori alimbatiza Tiridates III pamoja na maofisa wa ikulu na masharifu mbalimbali. Mfalme alitoa pia hati ya kumruhusu kabisa Gregori aongoe nchi nzima. Hivyo mwaka uleule Armenia ikawa taifa la Kikristo.[8]
Kanisa mama la Etchmiadzin, lililojengwa huko Vagharshapat, limebaki hadi leo kiini cha kanisa na taifa la Armenia.
Mwaka 302, Gregori aliwekwa wakfu na rafiki yake wa utotoni Leontius wa Kaesarea kama Patriarki wa Armenia[9].
Sikukuu na nyimbo kadhaa za dini ya jadi ziligeuzwa kuwa za Kikristo[10].
Mwaka 318, Gregori alimteua mwanae wa pili Aristaces kama mwandamizi[9] aeneze Ukristo katika Kaukazi. Pia alimuagiza mjukuu wake Gregori (bin Vrtanes) kufanya umisionari huko; hatimaye kijana huyo aliuawa akiwa anahubiri huko Albania ya Kaukazi.
Miaka ya mwisho Gregori alitawa pamoja na wachache wengine katika patakatifu karibu na Mlima Sebuh alipobaki hadi alipokufa[11].
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.