Jakaya Kikwete
Mwanasiasa wa Tanzania na raisi mstaafu From Wikipedia, the free encyclopedia
Mwanasiasa wa Tanzania na raisi mstaafu From Wikipedia, the free encyclopedia
Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa rais wa nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tangu tarehe 21 Desemba 2005 hadi tarehe 5 Novemba 2015.
Jakaya Mrisho Kikwete | |
Muda wa Utawala 21 Disemba 2005 – 5 Novemba 2015 | |
Makamu wa Rais | Ali M. Shein (2005–2010) Mohamed Bilal (2010–2015) |
---|---|
Waziri Mkuu | Edward Lowassa (2005–08) Mizengo Pinda (2008–2015) |
mtangulizi | Benjamin Mkapa |
aliyemfuata | John Magufuli |
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika | |
Muda wa Utawala 31 Januari 2008 – 2 Februari 2009 | |
mtangulizi | John Kufuor |
aliyemfuata | Muammar al-Gaddafi |
Muda wa Utawala Novemba 1995 – 21 Disemba 2005 | |
Rais | Benjamin Mkapa |
aliyemfuata | Asha-Rose Migiro |
Muda wa Utawala 1994 – 1995 | |
mtangulizi | Steven Kibona |
aliyemfuata | Simon Mbilinyi |
Mbunge wa Tanzania wa jimbo la Chalinze | |
Muda wa Utawala Novemba 1995 – 2005 | |
aliyemfuata | Ramadhani Maneno |
tarehe ya kuzaliwa | 7 Oktoba 1950 Msoga, Tanganyika |
utaifa | Mtanzania |
chama | CCM |
chamakingine | TANU |
ndoa | Salma Kikwete |
watoto | 8 |
makazi | Ikulu, Dar es Salaam |
mhitimu wa | Chuo Kikuu cha Dar es Salaam |
Fani yake | Mchumi |
dini | Uislamu |
Military service | |
Allegiance | Jamhuri ya Muungano wa Tanzania |
Service/branch | Jeshi la Tanzania |
Rank | Major |
Amezaliwa 7 Oktoba 1950 katika kijiji cha Msoga, kata ya Lugoba, tarafa ya Msoga, jimbo la uchaguzi la Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo, mkoa wa Pwani.
Lugha ya mama ilikuwa Kikwere.
Alizaliwa katika familia ya wanasiasa. Babu yake Mzee Mrisho Kikwete alikuwa chifu wa Wakwere. Baba yake alikuwa Mkuu wa Wilaya Pangani, Same na Tanga.
Jakaya Kikwete amesimulia hadithi ya kifamilia ya kuwa wakati mama yake alipokuwa mja mzito naye, babu alitamka kuwa ikiwa mtoto atakuwa wa kiume atampatia urithi wa cheo chake.
Miaka 1958 – 1961 akasoma Shule ya Msingi Msoga, halafu 1962 – 1965 Shule ya Kati (Middle School) Lusonga, halafu Shule ya Sekondari Kibaha akiongeza A-level huko Shule ya Sekondari Tanga.
Kuanzia mwaka 1972 alisoma uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akimaliza kwa kupata digrii yake mwaka 1978.
Akajiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Jakaya aliposoma Shule ya Sekondari ya Kibaha alikuwa mwenyekiti wa wanafunzi na pia wa Vijana wa TANU. Katika Shule ya Sekondari Tanga alikuwa Kiranja Mkuu na pia kiongozi wa timu ya mpira. Katika UDS alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa halmashauri ya wanafunzi.
1mwaka huu alikuwa mkulima wa Msoga. Mwaka 1988 akateuliwa kuwa mbunge na waziri msaidizi. Mwaka 1990 alichaguliwa kuwa mbunge wa Bagamoyo/Chalinze akirudishwa kila uchaguzi hadi mwaka 2000. Akawa waziri akipita katika wizara za maji na fedha.
Mwaka 1995 alijaribu kuchaguliwa kuwa mgombea wa urais upande wa CCM. Inasemekana ya kwamba Mwalimu Julius Nyerere alimwomba wakati ule kumwachia nafasi Benjamin Mkapa aliyeteuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM. Kikwete akawa Waziri wa Mambo ya Nje katika serikali zote mbili za Mkapa.
Mwaka 2005 alifaulu kuteuliwa mgombea wa CCM kwa nafasi ya rais akashinda uchaguzi wa Desemba 2005 akizoa 80% za kura zote.
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 alitangazwa tena mshindi ingawa kwa asilimia ndogo zaidi na kwa wasiwasi kuhusu uwezekano wa matokeo kuchakachuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi aliyoiteua mwenyewe. Katiba ya nchi hairuhusu kukata rufaa dhidi ya tangazo la tume hiyo.
Kuapishwa kwa mara ya kwanza kwa Jakaya Kikwete kama Rais wa 4 wa Tanzania kulifanyika Jumatano, tarehe 21 Desemba 2005. Ilikuwa ni mwanzo wa muhula wa kwanza wa miaka mitano wa Jakaya Kikwete kama Rais na Ali Mohamed Shein kama Makamu wa Rais.
Katika miaka mitano iliyofuata, rais aliendelea kusafiri sana nje ya nchi, kiasi kwamba alikaa ughaibuni siku nyingi kuliko zile alizokaa nchini Tanzania.
Hali ya mwisho ya nchi ilifananishwa na mwandamizi wake John Magufuli kuwa kama "shamba la bibi", ambamo kila mtu anaweza kuchuma anavyotaka. Pia rais mpya alilalamika kwa kukuta hazina haina fedha, mbali na madeni ya kimataifa kufikia kiasi cha karibu Shilingi za Tanzania milioni 1 kwa kila mwananchi.
Nishani | Nchi | Tarehe | Ref | |
---|---|---|---|---|
Nishani Ubora wa Lulu ya Afrika (Bwana tukufu) | Uganda | Julai 2007 | [1] | |
Nishani ya Hilali Kijani ya Komori | Komori | Machi 2009 | [2] | |
Nishani ya Abdulaziz Al Saud | Saudi Arabia | Aprili 2009 | [3] | |
Nishani ya Ubora | Jamaika | Novemba 2009 | [4] | |
Nishani ya Oman (Daraja la Kwanza) | Omani | Oktoba 2012 | [5] |
Chuo Kikuu | Nchi | Shahada ya Uzamivu | Tarehe | Ref |
---|---|---|---|---|
Chuo Kikuu cha Mtakatifu Thomas (Minnesota) | Marekani | Daktari wa Sheria | 28 Septemba 2006 | [6][7] |
Chuo Kikuu cha Kenyatta | Kenya | Shahada ya Heshima | 19 Disemba 2008 | [8] |
Chuo Kikuu cha Fatih | Uturuki | Shahada ya Heshima katika Mahusiano wa Kimataifa | Februari 2010 | [9] |
Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Muhimbili | Tanzania | Daktari wa Afya ya Umma | Disemba 2010 | [10] |
Chuo Kikuu cha Dodoma | Tanzania | Shahada ya Heshima | 26 Novemba 2010 | [11] |
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam | Tanzania | Daktari wa Sheria | Oktoba 2011 | [12] |
Chuo Kikuu cha Guelph | Kanada | Daktari wa Sheria | 20 Septemba 2013 | [13][14] |
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania | Tanzania | Shahada ya Heshima | 21 Januari 2016 | [15] |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.