Remove ads
From Wikipedia, the free encyclopedia
Amiri Muammar al-Gaddafi (kwa Kiarabu:معمر القذافي Mu‘ammar al-Qadhāfī) alikuwa kiongozi wa taifa la Libya.
| |
Kiongozi wa mapinduzi | |
Tarehe ya kuzaliwa | 1942 |
Mahali pa kuzaliwa | Sirte |
Tarehe ya kifo | 20 Oktoba 2011 |
Alingia ofisini | 8 Septemba 1969 |
Alitanguliwa na | Mfalme Idris I wa Libya |
Dini | Uislamu |
Alizaliwa katika familia ya mabedawi (wafugaji wa kuhamahama) mnamo mwaka 1942.
Baada ya masomo ya sheria kwenye chuo kikuu cha Libya alijiunga na jeshi mwaka 1963 akasoma kwenye chuo cha kijeshi cha Sandhurst (Uingereza) mwaka 1965.
Tarehe 1 Septemba 1969 pamoja na maafisa wenzake alipindua serikali ya mfalme Idris I na kutangaza Jamhuri ya Kiarabu ya Libya.
Ingawa hakuwa na cheo rasmi aliendelea kutawala nchi yake akiitwa "Kiongozi wa mapinduzi ya 1 Septemba ya Jamahiriya ya Ujamaa ya watu ya Kilibya-Kiarabu".
Hatimaye akapinduliwa mwenyewe tarehe 23 Agosti 2011, na kuuawa tarehe 20 Oktoba 2011.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Muammar al-Gaddafi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.