Chalinze ni jina la mji mdogo ambayo imekuwa makao makuu ya Wilaya ya Chalinze katika Mkoa wa Pwani, Tanzania. Eneo la mji linaundwa na kata za Bwilingu (Chalinze yenyewe) na Pera.

Ukweli wa haraka Nchi, Mkoa ...
Mji Mdogo wa Chalinze
Nchi Tanzania
Mkoa Pwani
Wilaya Chalinze
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 48,000
Funga

Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata hizo mbili zilikuwa na wakazi wapatao 48,000 walioishi humo. [1]

Chalinze iko km 110 kutoka Dar es Salaam. Inajulikana kama njiapanda muhimu kwenye barabara kuu za Tanzania. A14 ya kwenda Kilimanjaro na Tanga inaachana hapa na A7 ya kuelekea Morogoro - Iringa ikiendelea kama A104 hadi Mbeya - Zambia/Malawi. Kwa madereva ni maarufu kwa sababu polisi wa barabarani hupima mwendokasi wa magari kwa kutumia mitambo na wengi wanalazimika kulipa faini.

Shughuli kuu za kiuchumi katika mji huo ni kilimo cha mazao ya chakula na biashara, pia ufugaji unafanyika kwa kiwango kidogo.

Mji wa Chalinze haujawahi kuandaliwa Mpango wa Jumla kwa ajili ya kusimamia, kuongoza na kudhibiti matumizi ya ardhi ya mji huo kulingana na Sheria ya Mipangomiji namba 8 ya mwaka 2007.

Changamoto zinazokabili Mji wa Chalinze

Mji wa Chalinze, kama ilivyo katika miji mingi nchini, unakabiliwa na changamoto mbalimbali za kiuchumi, kijamii na kimazingira zinazosababisha mji huo kukua holela. Changamoto hizo ni pamoja na zifuatazo:

  • Kuwepo kwa ongezeko kubwa la idadi ya watu ikilinganishwa na uwezo wa mamlaka ya upangaji kukidhi mahitaji ya upangaji, upimaji wa viwanja na uwekaji wa miundombinu na huduma za jamii.
  • Kutokuwepo kwa mipango ya jumla na ya kina ya usimamizi wa mipango ya mji na udhibiti wa uendelezaji maeneo ya mji. Hii ni pamoja na kutokuwepo kwa rasilimali fedha za kutosha kwa ajili ya kuandaa mipango ya kusimamia uendelezaji wa mji na kudhibiti ukuaji wake (Mipango ya Jumla).
  • Kuwepo kwa ongezeko la ujenzi holela na hivyo kuwa na makazi ambayo hayajapangwa inayosababishwa na kukosekana kwa mipango na kasi ndogo ya upimaji wa ardhi kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwemo makazi, biashara, viwanda, uwekezaji, matumizi ya umma, n.k.
  • Ongezeko la vijiji vinavyokua haraka na kuchukua sura ya kimji. Vijiji hivyo vinakua bila ya kuwa na mipango inayowezesha kutoa dira ya uendelezaji wa kimji na hivyo kusababisha kuendelezwa holela.
  • Ushiriki mdogo wa sekta binafsi katika kupanga na kuendeleza miji.

Marejeo

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.