From Wikipedia, the free encyclopedia
Wilaya ya Chalinze ni mojawapo ya wilaya nane za Mkoa wa Pwani, Tanzania. Wilaya hiyo inapakana na Wilaya za Handeni na Pangani upande wa kaskazini na upande wa kusini na Wilaya za Bagamoyo na Kibaha. Magharibi iko Morogoro Vijijini na upande wa mashariki wilaya inapakana na Bahari ya Hindi.
Maeneo yake yalitengwa mwaka 2015 na Wilaya ya Bagamoyo na halmashauri yake ilianza kufanya kazi rasmi mwezi Julai 2016 [1].
Eneo la Wilaya ya Chalinze ni km2 8,042 zinazolingana na hekta 804,200. Takribani hekta 404,859 zinatumika kwa shughuli za kilimo na mifugo na hekta 51,127 ni misitu ya hifadhi za vijiji. Hifadhi za Saadani na Wami zinapatikana ndani ya wilaya hiyo.
Tabianchi ni ya kitropiki na kiwango cha mvua ni kati ya mm 800 hadi 1200 kwa mwaka. Mvua za vuli zinaanza kati ya mwezi Machi hadi katikati ya mwezi Mei. Majira ya kiangazi yanaanza katikati ya mwezi Mei hadi Oktoba.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 316,759 [2].
Makao makuu yapo mjini Chalinze.
Pamoja na Bagamoyo misimbo ya posta huanza kwa 613.
Barabara muhimu za A7 (TANZAM) na A14 zinapita humo zikikutana mjini Chalinze.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.