Mwalimu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mwalimu (kutoka neno la Kiarabu; kwa Kiingereza teacher, school teacher na pengine educator) ni mtu anayesaidia wengine kupata ujuzi, maarifa na tunu.


Kazi hiyo inaweza kufanywa na yeyote katika nafasi maalumu, kwa mfano mzazi au ndugu akimfundisha mtoto nyumbani, lakini kwa wengine ndiyo njia ya kupata riziki inayomdai karibu kila siku kwa miaka mingi, kwa mfano shuleni. Huko mwalimu anatakiwa kuwa na shahada au stashahada, kadiri ya sheria za nchi na ya ngazi ya elimu inayotolewa.
Imesemekana kuwa walimu vijana wanafundisha kuliko wanavyojua, yaani hata mengi wasiyoyajua vizuri. Wenye umri wa makamo wanafundisha yale yote wanayoyajua. Kumbe wazee wanafundisha yale yanayowafaa wasikilizaji.
Majukumu

Majukumu ya mwalimu yanaweza kutofautiana kadiri ya utamaduni husika.[1][2]
Mara nyingi ni pamoja na kufundisha kusoma na kuandika, kuhesabu, kufanya kazi fulani ya mikono, kushirikiana katika jamii, kufuata dini, kuunda kazi za sanaa.
Kwa kawaida ufundishaji huo unadai mwalimu aandae somo kwa kufuata mtaala fulani, kutoa vipindi na kutathmini maendeleo ya mwanafunzi. Pia ni muhimu atunze nidhamu.
Nje ya madarasa, pengine mwalimu anatakiwa kuongoza wanafunzi wake katika safari za kutembelea mashamba, viwanda, kumbi, makumbusho, n.k.
Sifa zinazohitajika
Ualimu ni kazi ngumu sana, kwa sababu unahusika na mambo mengi.[3][4][5]
Umoja wa Ulaya umetaja sifa tatu muhimu:
- Uwezo wa kushirikiana na wengine
- Uwezo wa kutumia ujuzi, teknolojia na habari, na
- Uwezo wa kufanya kazi ndani na pamoja na jamii.[6]
Wataalamu wa sayansi ya elimu wanazidi kukubaliana kwamba mwalimu yeyote anahitaji mambo matatu:
- ujuzi (kufahamu mada na namna ya kuifundisha, mtaala, sayansi ya elimu, saikolojia, tathmini n.k.)
- vipaji (kupanga kipindi, kutumia vifaa, kuongoza wanafunzi, kuendesha makundi, kutathmini maendeleo) na
- misimamo (tunu, tabia, imani na uwajibikaji).[7]
Walimu maarufu
- Edith Abbott
- Howard Adelman
- Raymond Macdonald Alden
- Henry James Anderson
- Charles William Bardeen
- Lancelot Bavin
- Juan Pablo Bonet
- Yohane Bosco
- Leib Glantz
- Yohane Mbatizaji de La Salle
- Maria Montessori
- Charles Rollin
- Charles Wedemeyer
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.