![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/c/c3/Bundesarchiv_Bild_146-1987-074-16%252C_Dietrich_Bonhoeffer.jpg/640px-Bundesarchiv_Bild_146-1987-074-16%252C_Dietrich_Bonhoeffer.jpg&w=640&q=50)
Dietrich Bonhoeffer
From Wikipedia, the free encyclopedia
Dietrich Bonhoeffer (4 Februari 1906 - 9 Aprili 1945) alikuwa mchungaji wa Kilutheri, mwanatheolojia na mpinzani wa ufashisti, na mwanzilishi mmojawapo wa "Kanisa la Ungamo" nchini Ujerumani. Maandishi yake juu ya jukumu la Ukristo katika ulimwengu wa kisasa yamekuwa na ushawishi mkubwa, hasa kitabu chake Gharama ya Uanafunzi.[1]
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/c/c3/Bundesarchiv_Bild_146-1987-074-16%2C_Dietrich_Bonhoeffer.jpg/320px-Bundesarchiv_Bild_146-1987-074-16%2C_Dietrich_Bonhoeffer.jpg)
Mbali na maandiko yake ya kitheolojia, Bonhoeffer alijulikana kwa upinzani wake mkali dhidi ya udikteta wa Nazi, pamoja na kupinga mradi wa serikali wa kuua wagonjwa na siasa ya Hitler ya kutesa Wayahudi. [2]
Bonhoeffer alikamatwa mnamo Aprili 1943 na kufungwa katika gereza la Tegel kwa mwaka mmoja na nusu. Baadaye, alihamishiwa kwenye kambi ya wafungwa ya Flossenbürg.
Baada ya jaribio la kumwua Adolf Hitler kwenye tarehe 20 Julai 1944 alishtakiwa kushiriki katika maandalizi. Alihukumiwa haraka pamoja na washtakiwa wengine, wakiwemo maafisa wa kitengo cha ujasusi wa jeshi, kisha akanyongwa tarehe 9 Aprili 1945 siku chache kabla ya utawala wa Wanazi kuanguka.