Gereza
Sehemu ambayo watu wanaweza kufungwa kama sehemu ya kutumikia adhabu From Wikipedia, the free encyclopedia
Sehemu ambayo watu wanaweza kufungwa kama sehemu ya kutumikia adhabu From Wikipedia, the free encyclopedia
Gereza (pia: jela kutoka Kiingereza: jail au prison) ni mahali ambako watu wanalazimishwa kukaa wakishikwa kinyume cha matakwa yao.
Kwa kawaida hali ya kufungwa ndani ya gereza ni adhabu iliyotolewa na mahakama kwa mtu aliyevunja sheria. Mara nyingi watu hufungwa ndani pia wakishtakiwa tu kuvunja sheria wakisubiri kesi zao zisikiwe mahakamani.
Katika nchi kadhaa serikali inatumia gereza kufunga watu wanaopinga viongozi wa nchi au kukosoa serikali.
Asili ya neno la Kiswahili "gereza" ni Kireno "igreja" inayomaanisha "kanisa" (la Kikristo). Maana imebadilika kwa sababu makanisa ya kwanza ya Wareno katika Afrika ya Mashariki yalijengwa ndani ya maboma yao. Kwa hiyo ilhali "igreja" ya Wareno ilikuwa ndani ya jengo imara ya ngome ilitokea kwamba ngome yenyewe ikaitwa hivyo. Hapo neno jipya "gereza" lilikuwa na maana ya "boma, ngome". Baadaye ngome hizo hazikuwa tena na kazi ya kijeshi kutokana na maendeleo ya teknolojia ya silaha, hivyo zilitumiwa kama jela kutunza wafungwa. [1]
Neno "jela" limekopwa kutoka Kiingereza "jail" wakati wa ukoloni wa Kiingereza.
Gereza kimsingi ni jengo linalolindwa na lenye kuta nene, milango imara na madirisha yenye nondo zinazozuia kupita. Mara nyingi gereza huwa na majengo mbalimbali katika eneo kubwa lililoviringishwa kwa ukuta au fensi ya miiba. Nyumba za wafungwa ziko pamoja na ofisi za walinzi, mara nyingi pia karakana ambako wafungwa wanafanya kazi, nyumba ya jikoni na mengine. Minara inakaliwa na walinzi.
Vyumba vya wafungwa ni tofauti kati ya gereza na gereza; kuna vyumba ambako wafungwa wengi hushikwa pamoja; kuna vyumba vya wafungwa wawili-wawili. Nchi zinazofuata haki za binadamu hulenga kumpa kila mfungwa chumba chake cha pekee akiwa na nafasi ya kukutana na wafungwa wengine, kama kazini, wakati wa chakula au kwenye vipindi vya michezo. Kumtenga kabisa mfungwa na wafungwa wengine ni adhabu ya nyongeza.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.