Kampuni ya Teknolojia ya Marekani From Wikipedia, the free encyclopedia
Amazon.com, Inc. (inafanya biashara kama Amazon) ni kampuni ya Marekani yenye makao makuu Seattle, Washington, ambayo ilianzishwa na Jeff Bezos tarehe 5 Julai 1994.
Kampuni hiyo ndiyo kampuni kubwa kabisa duniani ya uuzaji wa bidhaa kwenye intaneti. Kwa kipimo cha mapato na mtaji wa soko, na ni ya pili baada ya Alibaba Group kwa jumla ya mauzo.
Tovuti ya amazon.com ilianza kama duka la vitabu mtandaoni na baadaye ilianza kuuza video, muziki, michezo ya video, nguo, samani, vyakula, vito n.k.
Kampuni hiyo pia inamiliki kampuni ya kuchapisha, Amazon Publishing, studio ya filamu na televisheni, Amazon Studios, inatengeneza bidhaa za elektroniki kama vile Kindle, Echo n.k.
Amazon ina maduka ya rejareja katika nchi za Marekani, Uingereza, Ireland, Ufaransa, Canada, Ujerumani, Italia, Hispania, Uholanzi, Australia, Brazili, Japan, China, India, Mexico, Singapore na Uturuki.
Mnamo mwaka 2015, Amazon iliipita kampuni ya Walmart kama kampuni ya uuzaji wa rejareja yenye thamani kubwa zaidi nchini Marekani. Amazon ni kampuni ya pili ya thamani zaidi duniani (nyuma ya Apple tu), kampuni kubwa ya intaneti kwa mapato duniani, na baada ya Walmart, mwajiri wa pili mkubwa nchini Marekani.
Mwaka wa 2017, Amazon ilinunua Whole Foods Market kwa $ bilioni 13.4. Mnamo Septemba 4, 2018, Amazon ilikuwa na thamani ya dola za Marekani trilioni 1.
Amazon inamiliki zaidi ya kampuni tanzu 40, ikiwa ni pamoja na Zappos, Shopbop, Diapers.com, Kiva Systems (sasa inaitwa Amazon Robotics), Audible, Goodreads, Teachstreet na IMDb.[1]
A9.com ni kampuni inayojihusisha na utafiti na teknolojia tangu mwaka 2003. [2]
Amazon Maritime, Inc. ni kampuni inayomiliki meli zinazosafirisha bidhaa za Amazon toka China hadi Marekani.[3]
Amazon Translate ni kampuni inayotumia teknolojia ya mashine ya kutafsiri.
Audible.com ni kampuni inayouza bidhaa za burudani ya masikioni kama vile vitabu, vipindi vya televisheni, n.k. Amazon iliinunua kampuni hii kwa dola za Kimarekani milioni $300.[4]
CreateSpace ni kampuni inayotoa huduma kwa waandishi, wachapishaji, watengeneza filamu na kampuni za muziki. Kampuni hii ilikuwa kampuni tanzu ya Amazon mwaka 2009.[5]
Whole Foods Market ni kampuni inayouza vyakula visivyo na kemikali zenye kuleta madhara kwa binadamu. [6]
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.