Uislamu nchini Guinea

From Wikipedia, the free encyclopedia

Uislamu nchini Guinea

Uislamu nchini Guinea ni dini yenye wafuasi wengi nchini humo, kukiwa na makadirio ya asilimia 85 ya wakazi wote wa Guinea kuwa ni Waislamu, hasa kwa mujibu wa takwimu yao ya mwaka wa 2005.

Uislamu kwa nchi

Wengi wao ni wafuasi wa dhehebu la Sunni wanaofuata mafunzo ya Maliki na mila zake pamoja na Qadiria na Tijani katika miongozo ya Sufi. Vilevile kuna nyendo za Ahmadiyya nchini humo.[1]

Ijapokuwa Wafaransa walianzisha koloni lao mnamo mwaka wa 1891, udhibiti wao dhidi ya kanda ulikuwa dhaifu mno.

Baada ya uhuru mnamo mwaka 1958, kiongozi Muislamu mwenye kufuata sera za Umarksi, Rais Sékou Touré hakupenda suala la kuendeleza Uislamu; hadi hapo uongozi na sifa ilivyoanza kwenda kombo kwenye miaka ya 1970 Touré ndipo akaomba taasisi za Kiislamu zirudishe uhusiano wake na serikali ili kuhalalisha utawala wake.

Tangu kifo cha Touré mnamo 1984, ushirikiano baina ya jumuia za Kiislamu na serikali uliendelea.[2]

Marejeo

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.