Uislamu barani Afrika

From Wikipedia, the free encyclopedia

Uislamu barani Afrika

Uislamu barani Afrika una uwepo mkubwa huko Afrika Kaskazini, Pembe ya Afrika, Pwani ya Waswahili, na wengine wengi huko Afrika Magharibi, kukiwa na idadi ndogo Afrika Kusini.

Thumb
Msikiti wa Taifa wa Abuja huko mjini Abuja, Nigeria.
Thumb
Larabanga Mosque huko Ghana (karne ya 13), mmoja kati ya miskiti ya zamani zaidi iliyodumu hadi leo Afrika Magharibi.
Thumb
Sankore Madrasah, Timbuktu, Mali (karne ya 12).

Uenezi wa Uislamu

Afrika ilikuwa bara la kwanza nje ya Uarabuni ambapo Uislamu lilianza kuenea mapema katika karne ya 7. Karibia theluthi moja ya idadi ya Waislamu wote duniani wanaishi katika bara hili.

Waislamu walipita Jibuti na Eritrea kuomba hifadhi ya makazi katika Ethiopia ya leo wakati wa Kuhamia Uhabeshi.[1]

Waislamu walio wengi barani Afrika ni wa dhehebu la Sunni; utatanishi wa Uislamu barani Afrika umeonekana katika shule mbalimbali za fikira, mapokeo, na sauti kutoka katika nchi nyingi za Afrika. Uislamu wa Afrika sio tuli kabisa na umekuwa ukibadilika kulingana na jamii ulionea - hasa kutokana na uchumi na hali za siasa.

Ilipata kukadiriwa mnamo mwaka wa 2002 ya kwamba taasisi za Kiislamu zimefikia asilimia 45 ya wakazi wote wa Afrika.[2]

Soma zaidi

  • J. Spencer Trimingham, History of Islam in West Africa. Oxford University Press, 1962.
  • Nehemia Levtzion and Randall L. Pouwels (eds). The History of Islam in Africa. Ohio University Press, 2000.
  • David Robinson. Muslim Societies in African History. Cambridge University Press, 2004.
  • Bruce S. Hall, A History of Race in Muslim West Africa, 1600-1960. Cambridge University Press, 2011, ISBN 9781107002876.
  • Paul Schrijver, Bibliography on Islam in contemporary Sub-Saharan Africa. African Studies Centre, Leiden, 2006, ISBN 9789054480679 Updated online version Ilihifadhiwa 7 Oktoba 2023 kwenye Wayback Machine.

Marejeo

Viungo vya nje

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.