From Wikipedia, the free encyclopedia
Kwa matumizi mengine za jina hili angalia Songambele
Songambele ni kata ya Wilaya ya Kongwa katika Mkoa wa Dodoma, Tanzania yenye postikodi namba 41518[1].
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 23,342 [2]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na watu wapatao 17,712 waishio humo.
Ni miongoni mwa kata ambazo zinafanya vizuri katika kulima na kufuga. Mazao ambayo yanastawi kwa wingi ni karanga, mahindi, uwele, alizeti na mtama. Wakazi wapo mstari wa mbele katika kilimo cha umwagiliaji; kwa mfano kupitia umwagiliaji wanalima mbogamboga na baadhi mazao ya chakula kama vile mahindi.
Pia ni sehemu nzuri kwa kufanya biashara. Kuna wafanyabiashara wadogowadogo kama wauzaji nyama, nafaka na mifugo; pia lipo gulio la kila wiki, kuna maduka ya jumla na rejareja, n.k.
Ukiwa Songambele unaweza kufanya uwekezaji katika kilimo, biashara, kuanzisha shule za awali, kutoa huduma za afya kama vile maduka ya dawa na hospitali.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.