Nzega Mjini
From Wikipedia, the free encyclopedia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Nzega Mjini ilikuwa kata ya Wilaya ya Nzega katika Mkoa wa Tabora, Tanzania yenye postikodi namba 45401.
Nzega Mjini | |
Mahali pa Nzega Mjini katika Tanzania |
|
Majiranukta: 4°12′54″S 33°11′7″E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Tabora |
Wilaya | Nzega |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 34,744 |
Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 34,744 waishio humo.[1] Kwa sasa imegawiwa katika kata mpya kama vile Nzega Mjini Mashariki na Nzega Mjini Magharibi.
Kuna kivutio cha bwawa la Uchama ambapo kuna maji mengi: watu hupenda kwenda kutembelea huko; pia maji hutumika kwa shughuli mbalimbali kama kufulia, kumwagilia bustani, kujengea na kunyweshea ng'ombe kwa kuyachota na kuwapa.
Kuna mnada wa nguo na wanyama siku ya Jumamosi ushirika ambapo Wanyamwezi na watu wengine hukutana na kufanya shughuli ya kununua bidhaa. Kipindi cha mnada ni siku ambayo inavutia sana watu: kuna nyama rosti za mbuzi, kondoo na ng'ombe. Pia kuna vinywaji vingi kama soda, bia na juisi. Watu hupata starehe.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.