From Wikipedia, the free encyclopedia
Mtwara ni mji wa Tanzania ambao ni makao makuu ya Mkoa wa Mtwara wenye postikodi namba 63100 [1].
Mtwara | |
Mahali pa mji wa Mtwara katika Tanzania |
|
Majiranukta: 10°16′12″S 40°11′24″E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Mtwara |
Wilaya | Mtwara Mjini |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 146,772 |
Mtwara ni mji wa bandari kando ya Bahari Hindi karibu na mpaka wa Tanzania na Msumbiji.
Kiutawala Mtwara ni wilaya ya Mtwara mjini, umeunganishwa pamoja na mji wa kihistoria wa Mikindani katika halmashauri ya manisipaa.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 146,772 [2]. Kulingana na sensa ya mwaka 2002 idadi ya wakazi wake ilikuwa 92,602 [3] .
Mtwara ni mji mpya ulioanzishwa tangu 1947 mahali ambako kulikuwa na kijiji kidogo cha wavuvi tu. Waingereza waliotawala Tanganyika wakati ule walipanga mradi mkubwa wa kilimo katika Tanganyika ya Kusini wakahitaji bandari kwa ajili ya kubeba mazao yake. Mji ulipangwa kitaalamu kwa ajili ya wakazi 200,000 na mahali palichaguliwa kwa sababu ya bandari asilia iliyofaa hata kwa meli kubwa.
Bandari ilijengwa na mji mpya ulianzishwa lakini tangu 1950 ilionekana ya kwamba mradi wa kilimo kilishindikana. Mwaka 1953 mji ulikuwa na wakazi 36,999 pekee. Mji haukuendelea, ukarudi nyuma hasa kwa sababu pwani ya Kusini ilikosa barabara na njia za mawasiliano. Vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Msumbiji ilizuia biashara ya mpakani.
Tangu miaka ya 1990 uchumi ulianza kusonga mbele polepole. Barabara ya lami inaendelea kutengenezwa kutoka Dar es Salaam kuelekea Mtwara. Tangu kukamilishwa kwa daraja la mto Rufiji mawasiliano kwa barabara yameboreshwa hata wakati wa mvua. Vilevile feri inayovuka mto Ruvuma imeongeza biashara ya mpakani na Msumbiji.
Mtwara ni kitovu cha usafiri katika kusini-mashariki ya Tanzania. Mabasi kadhaa hufika kila siku kutoka Dar es Salaam. Meli hufika mara kwa mara. Uwanja wa ndege hufikiwa na Air Tanzania mara tano kwa wiki. Barabara ya lami imefikia Lindi na Masasi. Feri ya mto Ruvuma inabeba magari na mizigo karibu kila siku. Daraja kwenda Msumbiji unapangwa.
Kuna pia mipango ya kujenga barabara imara ya lami kutoka Mtwara kwenda Songea na Ziwa Nyasa itakayowezesha bandari ya mji kuhudumia kusini mwote mwa Tanzania pamoja na Malawi.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.