Remove ads
nchi katika Ulaya Kusini-Magharibi From Wikipedia, the free encyclopedia
Uhispania (Kihispania: España; Kiingereza: Spain) ni nchi ya Ulaya ya kusini-magharibi. Imepakana na Ufaransa, Andorra, Ureno na eneo la Kiingereza la Gibraltar.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Plus Ultra (Kilatini kwa "Mbele na zaidi") | |||||
Wimbo wa taifa: Marcha Real au Marcha Granadera | |||||
Mji mkuu | Madrid | ||||
Mji mkubwa nchini | Madrid | ||||
Lugha rasmi | Kihispania(1) | ||||
Serikali Mfalme Waziri Mkuu |
Ufalme wa kikatiba Felipe VI Pedro Sánchez | ||||
Kuungana kwa nchi Kungana kwa ndoa za wafalme Maungano Hali halisi Kisheria |
1516 1716 1812 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
504,782 km² (ya 50) 1.04% | ||||
Idadi ya watu - 2018 kadirio - 2001 sensa - Msongamano wa watu |
46.733.038 (ya 30) 40,847,371 92/km² (ya 112) | ||||
Fedha | Euro (€)(2) (EUR ) | ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
CETKigezo:Footnote (UTC+1) CEST (UTC+2) | ||||
Intaneti TLD | .es | ||||
Kodi ya simu | +34
- | ||||
Kigezo:Fnb Majimbo ya kujitawala ya Hispania yanatumia lugha za: Kikatalunya/Kivalencia, Kibaski na Kigalicia pamoja na Kihispania. Katika Bonde la Val d'Aran lahaja ya Kiarani ya lugha ya Kioksitani ni lugha rasmi pamoja na Kihispania; Kigezo:Fnb Hadi 1999: Peseta Kigezo:Fnb Ispokuwa Visiwa vya Kanari |
Kuna pwani ndefu ya Bahari ya Mediteranea na pia ya Atlantiki.
Uhispania bara ni sehemu kubwa ya rasi ya Iberia. Visiwa vya Baleari kwenye Mediteranea na Visiwa vya Kanari katika Atlantiki pamoja na miji ya Afrika ya Kaskazini Ceuta na Melilla ni sehemu za Uhispania.
Mji mkuu ni Madrid ambayo ni pia mji mkubwa wa nchi.
Eneo la nchi ni km² 505,990 nalo lina wakazi 47,450,795 (sensa ya mwaka 2020).
Mfalme Felipe VI amevaa taji mwaka 2014, akishika nafasi ya baba yake Juan Carlos I, anayeheshimiwa sana kwa sababu aliongoza taifa katika mabadiliko ya kutoka udikteta wa jenerali Francisco Franco kuelekea demokrasia. Hasa tendo la mfalme la kuzuia mapinduzi wa kijeshi linakumbukwa sana.
Muundo wa serikali ni Ufalme wa Kikatiba, hivyo kisheria madaraka ya mfalme ni madogo.
Utawala umo mikononi mwa serikali inayochaguliwa na bunge linaloitwa "Las Cortes likichaguliwa kwa kura za kidemokrasia.
Wakazi wa kwanza waliojulikana kwa jina kuwa waliishi Uhispania walikuwa Wakelti.
Katika karne za KK Wafoinike walianzisha miji kwenye pwani na kuchimba madini hasa shaba na fedha.
Waroma wa Kale walivamia na kutawala Uhispania kwa karne kadhaa wakileta lugha yao ya Kilatini kilichopata kuwa msingi wa lugha za kisasa za Uhispania. Kibaski pekee si lugha ya Kirumi.
Katika karne ya 5 makabila ya Kigermanik walivamia Dola la Roma pamoja na Uhispania. Kati yao Wavandali na Wavisigothi walitawala sehemu kubwa ya Uhispania.
Tangu mwaka 711 jeshi la Waarabu Waislamu liliingia kutoka Afrika ya Kaskazini na kutwaa sehemu kubwa ya Uhispania hadi karibu milima ya Pirenei, lakini watawala wa maeneo kadhaa katika kaskazini walijihami na kufaulu kudumisha uhuru wao.
Waarabu walileta fani nyingi za maendeleo nchini.
Katika kipindi cha vita cha karne nyingi Wakristo wa Kaskazini walifaulu polepole kuwarudisha nyuma Waarabu hadi kusini kwa nchi.
Hatimaye mwaka 1492 mfalme Boabdil wa Granada, mji wa mwisho wa Waarabu, alishindwa na mfalme Ferdinand II wa Aragon na malkia Isabella wa Kastilia.
Wiki chache kabla ya kushinda huko Granada wafalme wa Uhispania walimkubalia nahodha Kristoforo Kolumbus kutafuta njia ya kufika Bara Hindi kupitia magharibi. Badala ya kufika India Kolumbus alifika kwenye visiwa vya Amerika ya Kati.
Huo ulikuwa mwanzo wa upanuzi wa Uhispania katika "Dunia Mpya" ya Amerika. Wahispania walijenga dola kubwa la kikoloni na kutwaa karibu Amerika ya Kusini yote pamoja na Amerika ya Kati na Mexiko hadi sehemu za kusini za Marekani ya leo.
Katika miaka mia tatu iliyofuata Uhispania ilitajirika sana kutokana na maliasili ya Amerika.
Vita hivyo vilitokea mwaka 1898. Vilianza kwa shambulizi la Marekani tarehe 25 Aprili dhidi ya Puerto Rico vilivyokuwa koloni la Uhispania na kuishia tarehe 12 Agosti 1898, jeshi la Uhispania huko Manila (Ufilipino) liliposalimu amri.
Vita hivyo vilikuwa mwanzo wa Marekani kufuata siasa ya nje ya upanuzi hata katika maeneo ya mbali. Kabla ya vita hivyo Marekani ilishughulika kupanua eneo lake kwenye bara la Amerika ya Kaskazini dhidi ya wakazi asilia na dhidi ya Mexiko.
Marekani ilitumia nafasi ya ghasia ya wenyeji wa Kuba dhidi ya utawala wa kikoloni wa Uhispania.
Baada ya mlipuko kwenye manowari ya Marekani USS Maine katika bandari ya Havana, Marekani ilitangaza vita dhidi ya Uhispania ingawa sababu ya mlipuko haijajulikana hadi leo ilikuwa nini.
Uhispania haikuweza kushindana na manowari na silaha za Marekani zilizokuwa zimeendelea kiteknolojia.
Pia Marekani ilikuwa karibu na mahali pa vita na Uhispania ilishindwa kuongeza wanajeshi na silaha.
Hivyo Marekani ilitwaa makoloni ya Uhispania ya Puerto Rico, Kuba na Ufilipino.
Bendera | Jimbo la kujitawala | Mji mkuu wa jimbo | Rais wa jimbo | Bunge la jimbo | Vyama tawala jimboni | Viti katika seneti | Eneo(km2) | Wakazi (2019) | Msongamano (/km2) | GDP kwa mkazi (kwa euro) | Hali |
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Andalusia | Seville | Juan Manuel Moreno (PP) | Parliament of Andalusia | PP, Cs | 41 (9 RA,
32 DE) |
87,268 | 8,414,240 | 96 | 19,107 | Nationality | |
Catalonia | Barcelona | Pere Aragonès (Republican Left of Catalonia) | Parliament of Catalonia | ERC, Junts, PDeCAT (until 2020) | 24 (8 RA, 16 (DE) | 32,114 | 7,675,217 | 239 | 30,426 | Nationality | |
Jimbo la Madrid | Madrid | Isabel Díaz Ayuso (PP) | Assembly of Madrid | PP, C's (until 2021) | 14 (7 RA, 4 DE) | 8,028 | 6,663,394 | 830 | 35,041 | Region | |
Jimbo la Valencia | Valencia | Ximo Puig (PSOE) | Valencian Cortes | PSOE, Compromís, Unides Podem | 17 (5 RA, 12 DE) | 23,255 | 5,003,769 | 215 | 22,426 | Nationality | |
Galicia | Santiago de Compostela | Alberto Núñez Feijóo (PP) | Parliament of Galicia | PP | 19 (3 RA, 16 DE) | 29,574 | 2,699,499 | 91 | 23,183 | Nationality | |
Castilia na León | Valladolid (de facto seat of institutions) | Alfonso Fernández Mañueco (PP) | Cortes of Castile and León | PP, Cs | 39 (3 RA, 36 DE) | 94,223 | 2,399,548 | 25 | 24,031 | Historical region | |
Nchi ya Kieuskara | Vitoria-Gasteiz (de facto seat of institutions) | Iñigo Urkullu (PNV) | Basque Parliament | PNV, PSOE | 15 (3 RA, 12 DE) | 7,234 | 2,207,776 | 305 | 33,223 | Nationality | |
Castilla–La Mancha | Toledo | Emiliano García-Page (PSOE) | Cortes of Castilla–La Mancha | PSOE | 23 (3 RA, 20 DE) | 79,463 | 2,032,863 | 26 | 20,363 | Region | |
Visiwa vya Kanari | Santa Cruz de Tenerife and Las Palmas de Gran Canaria | Ángel Víctor Torres (PSOE) | Parliament of the Canary Islands | PSOE, NCa, Podemos, ASG | 14 (3 RA, 11 DE) | 7,447 | 2,153,389 | 289 | 20,892 | Nationality | |
Jimbo la Murcia | Murcia | Fernando López Miras (PP) | Regional Assembly of Murcia | PP, Cs (until 2021) | 6 (2 RA, 4 DE) | 11,313 | 1,493,898 | 132 | 21,269 | Region | |
Aragon | Zaragoza | Javier Lambán (PSOE) | Aragonese Corts | PSOE, Podemos, CHA, PAR | 14 (2 RA, 12 DE) | 47,719 | 1,319,291 | 28 | 28,151 | Nationality | |
Extremadura | Mérida | Guillermo Fernández Vara (PSOE) | Assembly of Extremadura | PSOE | 10 (2 RA, 8 DE) | 41,634 | 1,067,710 | 26 | 18,469 | Region | |
Visiwa vya Baleari | Palma | Francina Armengol (PSOE) | Parliament of the Balearic Islands | PSOE, Podemos-EUIB, Més | 7 (2 RA, 5 DE) | 4,992 | 1,149,460 | 230 | 27,682 | Nationality | |
Ufalme mdogo wa Asturias | Oviedo | Adrián Barbón (PSOE) | General Junta of the Principality of Asturias | PSOE | 6 (2 RA, 4 DE) | 10,604 | 1,022,800 | 96 | 22,789 | Historical region | |
Jimbo la Navarra | Pamplona | María Chivite (PSOE) | Parliament of Navarre | PSN, GBai, Podemos | 5 (1 RA, 4 DE) | 10,391 | 654,214 | 63 | 31,389 | Nationality | |
Cantabria | Santander | Miguel Ángel Revilla (PRC) | Parliament of Cantabria | PRC, PSOE | 5 (1 RA, 4 DE) | 5,321 | 581,078 | 109 | 23,757 | Historical region | |
La Rioja | Logroño | Concha Andreu (PSOE) | Parliament of La Rioja | PSOE, Podemos | 5 (1 RA, 4 DE) | 5,045 | 316,798 | 63 | 27,225 | Region |
R.A: Regionally appointed; D.E: Directly elected.
Bendera | Mji wa kujitawala | Meya | Halmashauri | Vyama tawala mjini | Viti katika seneti | Eneo (km2) | Wakazi (2019) | Msongamano (/km2) | GDP kwa mkazi (kwa euro) |
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Melilla | Eduardo de Castro (Cs) | Assembly of Melilla | CpM, PSOE, Cs | 2 (DE) | 12.3 | 86,487 | 7,031 | 16,981 | |
Ceuta | Juan Jesús Vivas (PP) | Assembly of Ceuta | PP | 2 (DE) | 18.5 | 84,777 | 4,583 | 19,335 |
Wakazi walio wengi (84.8%) ni Wahispania asili, lakini uhamiaji mkubwa wa miaka ya mwisho umeleta watu wengi hasa kutoka Amerika ya Kilatini, Afrika Kaskazini, Ulaya Mashariki n.k.
Lugha rasmi ni Kihispania inayozungumzwa nyumbani na 74% za watu lakini majimbo 17 yamepewa mamlaka ya kujitawala katika mambo mbalimbali pamoja na sera za kiutamaduni, hivyo lugha za Kikatalunya (17%), Kigalicia (7%), Kibaski (2%) na Kioccitan zimekuwa lugha rasmi za kijimbo pamoja na Kihispania.
Wahispania walio wengi (61%) ni waamini wa Kanisa Katoliki. 34% hawana dini yoyote.
Makala hii kuhusu maeneo ya Hispania bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Uhispania kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.