From Wikipedia, the free encyclopedia
Leopoldo Bogdan Mandić, O.F.M.Cap. (Herceg Novi, Boka Kotorska, Montenegro, 12 Mei 1866 - Padova, Italia, 30 Julai 1942) alikuwa kwa asili mtu wa kabila la Wakorasya.[1]
Ingawa mfupi sana (mita 1.35) na mlemavu, alistawi kiroho hasa baada ya kujiunga na utawa wa Ndugu Wadogo Wakapuchini na kufikia upadri (20 Septemba 1890).
Alitamani kwenda Ulaya Mashariki ili kurudisha umoja kati ya Wakatoliki na Waorthodoksi, lakini kwa utiifu aliishi karibu daima nchini Italia, na tangu mwaka 1906 hadi kifo chake alikuwa Padova akiungamisha mchana kutwa umati wa watu waliomuendea, wakivutiwa na wema wake[2].
Wakati wa Vita vikuu vya pili, mabomu yalibomoa konventi alimoishi na kanisa lake, lakini si chumba alimokuwa anaungamisha. Ndivyo alivyokuwa ametabiri, "Hapa Mungu ametumia sana huruma yake kwa watu wengi, lazima pabaki kama ukumbusho wa wema wake".
Papa Paulo VI alimtangaza mwenyeheri tarehe 2 Mei 1976, halafu Yohane Paulo II alimtangaza mtakatifu tarehe 16 Oktoba 1983.
Sikukuu yake huadhimishwa kila tarehe 30 Julai[3] au 12 Mei.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.