From Wikipedia, the free encyclopedia
Kwa maana nyingine, tazama Wilaya ya Iramba.
Iramba ni kata ya Wilaya ya Bunda katika Mkoa wa Mara, Tanzania yenye postikodi namba 31519.
Kata hiyo inazungukwa na maji pande kuu tatu ikiwa kama rasi iliyoingia katika ziwa Viktoria. Kwa upande wa majini imezungukwa na visiwa kama Ilela, Nyamigongo, Nyambugu, Igali, Burwa, Bugurani na Nyamasanje.
Kata ya Iramba ina vijiji vitano ambavyo ni Isanju, Mugara, Nyarugoma, Sikiro na Mwiruruma. Makao makuu ya kata yapo Isanju. Upande wa nchi kavu vijiji vyote vitano vinavyounda kata hiyo vinaunganishwa na safu ya milima ya Iramba.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 13,850 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 10,715 waishio humo.[2]
Jamii ya watu wa Iramba ni hasa ya makabila ya Wajita, Wasukuma, Wakerewe na Wajaluo. Wakazi wa kata wanajishugulisha hasa na kilimo, uvuvi, na ufugaji.
Kilimo: maeneo ya kilimo ndani ya kata yanafanyika katika mwambao wa ziwa na maeneo ya milimani (safu za milima ya Iramba). Wakulima wa maeneo hayo hushughulika na mazao ya muhogo, viazi vitamu, uwele na mtama kama mazao ya chakula; pia pamba, mahindi na mpunga kama mazao ya biashara.
Uvuvi: vijana wengi wa Iramba wanajishughulisha na uvuvi; samaki wanaovuliwa ni sato, sangara na dagaa. Maeneo yaliyoshamiri kwa uvuvi ni Mugara, Sikiro, Isanju na Nyarugoma, pamoja na maeneo ya visiwani kama Ilela, Nyamigongo na Igari ambavyo ni vivutio vya wavuvi katika kata ya Iramba.
Ufugaji: jamii ya Iramba wanajihusisha na ufugaji wa ng'ombe, mbuzi, kondoo na kuku.
Biashara: kuna wajasiriamali na vikundi mbalimbali vya wakina mama wanaojihusisha na ujasiriamali, pia wafanyabiashara wa samaki, mazao ya chakula, bidhaa mabalimbali na wafanyabiahara kutoka nje.
Vivutio vya Iramba:
Kivuko cha MV MARA huunganisha Iramba na Majita (wilaya ya Bunda na wilaya ya Musoma Vijijini).
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.