From Wikipedia, the free encyclopedia
Herodia (kwa Kigiriki Ηρωδιάς, Hērōdiás; (15 KK hivi — baada ya 39 BK) alikuwa mwanamke wa ukoo wa Herode huko Uyahudi chini ya himaya ya Dola la Roma.[1][2]
Ni maarufu hasa kwa kufanya mpango wa kumuua Yohane Mbatizaji hata akaufanikisha.
Herode Mkuu alipoua wanae Aleksanda na Aristobulo IV mwaka 7 KK, Herodia alibaki yatima, hivyo Herode alimuoza kwa mwanae Herode II.
Baadaye Herodia alitengana na mumewe ili aolewe na Herode Antipa, mtawala wa Galilaya na Perea.[5]
Herode II na Herodias walimzaa Salome (binti Herode).[6][7]
Kadiri ya Injili, Yohane Mbatizaji alifungwa na Herode Antipa kwa sababu ya kulaumu ndoa hiyo; hatimaye Herodia alifanya njama na binti yake Salome, akafaulu kumfanya Herode amkate kichwa Yohane.
Hatimaye Herode Antipa alinyang'anywa madaraka na kupelekwa uhamishoni sehemu za Ufaransa wa leo, ambako Herodia alimfuata.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.