Ubongo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Ubongo ndio kiini cha mfumo wa neva katika wanyama wote wenye ugwemgongo, na wengi wa wanyama wasio na ugwemgongo.[1] Baadhi ya wanyama wasiositawi, kama vile konyeza na kiti cha pweza, wana mfumo wa neva uliogatuliwa bila ubongo, huku tipwatipwa wa bahari wakikosa mfumo wa neva kabisa. Katika wanyama wenye ugwemgongo, ubongo umo katika kichwa ukilindwa na mifupa ya fuvu na ukiwa karibu na viungo vya hisia za msingi yaani kuona, kusikia, kugusa, ladha na harufu.
Ubongo unaweza kuwa changamani sana. Gamba la ubongo wa binadamu lina takribani neuroni bilioni 15-33, labda zaidi, kutegemea jinsia na umri,[2] zilizounganishwa na takribani miunganiko ya sinapsi 10,000 kila mmoja. Kila milimita ya kizio cha ukubwa wa gamba la ubongo lina takribani sinapsi bilioni moja.[3] Neuroni hizi huwasiliana na nyingine kwa njia ya fumwele ndefu za protoplazimu ziitwazo akzoni, ambazo hubeba mifuatano ya mipigo ya vichocheo vitwavyo matendo tarajiwa kuelekea sehemu mbali za ubongo au mwili na kulenga seli maalumu itakazovipokea.
Ubongo hudhibiti mifumo mingine ya viungo vingine vya mwili, iwe kwa kusisimua misuli au kwa kusababisha kutolewa kwa kemikali kama vile homoni ambayo ni homoni ya pituitari. Udhibiti huu kutoka mahali moja unaruhusu majibu ya haraka na yaliyoratibiwa kwa mabadiliko katika mazingira. Baadhi ya mwitikio wa kimsingi inawezekana bila ubongo: hata viumbe walio na chembe moja wanaweza kufasiri yaliyo katika mazingira na kutenda kulingana na mabadiliko hayo.[4] Tipwatipwa wa bahari, wasio na mfumo mkuu wa neva, wanaweza kujikunyata na hata kusonga kwa namana iliyotibiwa.[5] Katika wauti, uti wa mgongo wenyewe una viungo vya neva vinavyoweza kuanzisha tendohiaria pamoja na kuelekeza mifumo rahisi ya kusonga kama vile kuogelea au kutembea.[6] Hata hivyo, udhibiti changamani wa tabia kwa msingi ya mchango wa hisia tete unahitaji uwezo-unganishaji wa ubongo wa kati.
Licha ya maendeleo ya kasi ya sayansi, mengi kuhusu jinsi ubongo unavyofanya kazi bado ni siri. Majukumu ya neva na sinapsi zikiwa pekee sasa inaeleweka kwa undani makubwa, lakini jinsi yanavyoshirikiana katika majumuia ya maelfu au mamilioni imekuwa vigumu sana fumbua. Mbinu za uchunguzi kama vile unakili wa EEG na upigaji picha ubongo unaofanya kazi umetuambia kwamba utendaji wa ubongo unatendeka kwa utaratibu sana, huku kunakili kitengo kimoja kukiweza kufichua shughuli za neva moja, jinsi chembe moja inavyo inavyochangia michakato changamani haijulikani.[7]