From Wikipedia, the free encyclopedia
Pweza ni wanyama wa bahari wenye minyiri (mikono) minane inayobeba vikombe vya kumung'unyia na inayotumika kwa kukamata wanyama wadogo. Wana domo linalofanana na lile la kasuku ili kuseta gegereka na kome. Spishi nyingi huingiza sumu inayopooza mawino.
Pweza | ||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Pweza madoa-meupe | ||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||
| ||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||
Nusuoda 2, familia za juu 2 na familia 12:
| ||||||||||
Pweza hunaogelea kwa kuondoa maji kwa nguvu kupitia mrija (siphon) wake. Wanaweza kubadilisha rangi yao na pengine umbo wao ili kufanana na kinyume na kujificha kwa mawindo na maadui. Wakivumbuliwa huruka wakitoa ghubari la kiwi (maada kama wino) ili kukanganya adui.
Pweza wanaweza kushambulia watu lakini hii ni adimu. Wakichochewa wanauma kwa domo lao na wanatoa sumu, lakini spishi moja tu, pweza mizingo-buluu, ana sumu inayoweza kuua watu
Kiumbe huyu huliwa sana na watu waishio pembezoni mwa bahari kwa sababu ana nyama nzuri tu, ila huwa na chumvi nyingi.
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Pweza kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.