From Wikipedia, the free encyclopedia
Papa Pius X (Riese, Veneto, Italia Kaskazini, 2 Juni 1835 – Roma, 20 Agosti 1914) alikuwa Papa kuanzia tarehe 4/9 Agosti 1903 hadi kifo chake[1]. Alitokea Riese, Treviso, Italia[2].
Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Giuseppe Sarto.
Alimfuata Papa Leo XIII na kuvishwa taji la Kipapa tarehe 9 Agosti 1903, wa kwanza katika karne ya 20. Akafuatwa na Papa Benedikto XV.
Alitangazwa na Papa Pius XII kuwa mwenyeheri tarehe 3 Juni 1951, halafu mtakatifu tarehe 29 Mei 1954.
Kabla ya kuchaguliwa kama Papa, aliwahi kuwa paroko, askofu wa Mantova (tangu 1884, halafu Patriarki wa Venice (tangu 1893). Hivyo alikuwa na mang'amuzi mengi ya kichungaji.
Kwa kuwa katika uchaguzi makardinali walimpiga kura kwanza mwenzao Rampolla, lakini huyo aliwekewa kura ya turufu na Kaisari wa Austria-Hungaria, mara alipochaguliwa Pius X alifuta haki hiyo ya Kaisari na kuamua atengwe na Kanisa Katoliki yeyote atakayeingilia tena uchaguzi wa Papa.
Lengo lake lilifafanuliwa na kaulimbiu yake: "Instaurare omnia in Christo", yaani "Kukamilisha yote ndani ya Kristo". Alilitekeleza kwa unyofu, ufukara na nguvu, akihamasisha maisha ya Kikristo kati ya waumini kwa kuwapa nafasi ya kushiriki zaidi ekaristi takatifu, kwa kustawisha ubora wa liturujia na kwa kuhakikisha usahihi wa imani[4].
Kweli alijitahidi kuleta hali mpya katika Kanisa.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.