![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/6/65/Nate_dogg_rapradar_%2528cropped%2529.jpg/640px-Nate_dogg_rapradar_%2528cropped%2529.jpg&w=640&q=50)
Nate Dogg
From Wikipedia, the free encyclopedia
Nathaniel Dwayne Hale (anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Nate Dogg; Clarksdale, Mississippi, 19 Agosti 1969 - Long Beach, 15 Machi 2011) alikuwa rapa na mwimbaji wa muziki wa hip hop na R&B kutoka nchini Marekani. Alifahamika sana kwa uanachama wake katika kundi la rap lililokuwa na wasanii watatu la 213 na kazi zake za kujitegemea ambapo amepata kushirikiana na Dr. Dre, Warren G, Tupac na Snoop Dogg katika matoleo kadha wa kadha bab-kubwa ya wasanii hao. Nate Dogg ametoa albamu tatu za kujitegemea, G-Funk Classics, Vol. 1 & 2 mnamo 1998, Music and Me mnamo 2001 na Nate Dogg mnamo 2008.
Ukweli wa haraka Maelezo ya awali, Jina la kuzaliwa ...
Nate Dogg | |
---|---|
![]() | |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Nathaniel Dwayne Hale |
Amezaliwa | (1969-08-19)Agosti 19, 1969 Clarksdale, Mississippi, Marekani |
Amekufa | Machi 15, 2011 (umri 41) Long Beach, California, United States |
Aina ya muziki | Hip hop, West Coast hip hop, R&B, G-funk |
Kazi yake | Rapa, Mwimbaji |
Miaka ya kazi | 1990–2011[1] |
Studio | Death Row Elektra Doggystyle Atlantic |
Ame/Wameshirikiana na | 213, Snoop Dogg, Warren G, 2Pac, Dr. Dre, The Game, Proof, Eminem, 50 Cent, Tha Dogg Pound, Fabolous |
Funga