Kipandauso
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kipandauso ni tatizo linalotambulika kwa maumivu ya kichwa yanayojirudia tena makali hadi kiasi cha kupindukia na ambayo wakati mwingi huambatana na dalili nyingi za mfumo wa neva.
Migraine | |
---|---|
Mwainisho na taarifa za nje | |
Specialty | Neurology ![]() |
ICD-10 | G43. |
ICD-9 | 346 |
OMIM | 157300 |
DiseasesDB | 8207 (Migraine) 31876 (Basilar) 4693 (FHM) |
MedlinePlus | 000709 |
eMedicine | neuro/218 neuro/517 emerg/230 neuro/529 |
MeSH | D008881 |
Jina la Kiingereza "Migraine" limetoka katika neno la Kigiriki ἡμικρανία (hemikrania), "uchungu kwa upande mmoja wa kichwa",[1] kutoka ἡμι- (hemi-), "nusu", na κρανίον (kranion), "fuvu la kichwa".[2]
Kwa kawaida, maumivu hayo huathiri sehemu moja ya kichwa, huku kikidunda kwa muda wa saa 2 hadi 72. Dalili zinazohusiana na hali hii ni pamoja na kichefuchefu, kutapika, fotofobia, fonofobia (ongezeko la usikivu dhidi ya sauti) na uchungu wake kwa kawaida huzidishwa na shughuli za kimwili.[3] Hadi thuluthi moja ya watu wenye ugonjwa wa kipandauso kinachoandamana na maumivu ya kichwa hupata aura: ishara bandia ya matatizo ya macho, hisia, lugha au mwendo inayoashiria kuwa maumivu ya kichwa yatatokea punde.[3]
Kipandauso huaminika kutokea kufuatia mchanganyiko wa masuala ya kimazingira na kijeni.[4]Thuluthi mbili za kesi hizo zinahusika na familia.[5]
Kiwango cha homoni kinachoshuka na kupanda pia kinaweza kuwa kisababishi cha ugonjwa huu: kipandauso huathiri wavulana kwa kiwango cha juu kidogo kuliko wasichana kabla ya kubalehe, ingawa kinawaathiri wanawake mara mbili hadi tatu kuliko wanaume,[6][7] ila ujauzito unakipunguza.[6]
Utaratibu wa ugonjwa huu haujatambulika. Hata hivyo, hali hii inaaminika kuwa tatizo la mfumo wa neva.[5] Nadharia ya msingi inahusiana na kuongezeka kwa uchangamfu wa koteksi ya serebramu na udhibiti usio wa kawaida wa maumivu ya nyuroni kwa kiiniseli cha trijemia cha mfumo wa ubongo.[8]
Matibabu ya kwanza yanayopendekezwa ni dawa za kuondoa maumivu kama vile ibuprofen na acetaminophen ili kutuliza maumivu ya kichwa na antiemetic ili kutuliza kichefuchefu na kuepuka vichocheo. Dawa maalumu kama vile triptan au ergotamine zinaweza kutumika kwa watu wasiosaidiwa na dawa za kawaida za kuondoa maumivu. Zaidi ya asilimia 10 ya watu wote ulimwenguni huathiriwa na kipandauso wakati fulani maishani mwao.