Imani ya Kanisa
From Wikipedia, the free encyclopedia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Imani ya Kanisa (kwa Kilatini: fides Ecclesiae; kwa Kiingereza: Faith of the Church) ni wazo la msingi la teolojia ya Kanisa Katoliki. Maana yake ni kwamba imani si kazi ya Mkristo binafsi kwanza, bali ya Kanisa lote kwa pamoja[1].
Kanisa ndilo lilipokea amana au hazina ya imani (depositum fidei) kwa Yesu Kristo kupitia Mitume wake. Likiongozwa na Roho Mtakatifu, alivyoahidi Yesu mwenyewe (Yoh 16:12-14), Kanisa linazidi kukumbuka na kuelewa yale yote yaliyofunuliwa naye, ili kwamba yawe hai karne hata karne.
Hata yakitokea mapungufu au kukosekana uwiano mzuri katika ufundishaji wa imani wakati fulani au katika eneo fulani, Kanisa zima linasadikika kuwa haliwezi kupotewa na ukweli, bali linazidi kuufahamu kikamilifu.
Vilevile, tendo la Mkristo kumsadiki Mungu na ufunuo wake linabebwa na imani ya taifa lake lote kama mtoto anavyobebwa na mama yake na kufundishwa naye kujua na kusema.
Hivyo Mkatoliki anahimizwa kushiriki zaidi na zaidi imani ya Kanisa lote (la nyakati zote na la mahali kote) ili azidi kusadiki kwa hakika, mbali na tafsiri binafsi zinazoweza kuathiriwa na umimi, na utamaduni n.k.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.