nchi huru katika Afrika Magharibi From Wikipedia, the free encyclopedia
Gine, (pia: Gini; Kifaransa: Guinée; Kiingereza: Guinea) kirasmi Jamhuri ya Gine, ni nchi katika Afrika ya Magharibi. Pengine inatajwa kama Gine-Conakry ili kuitofautisha na nchi za Gine-Bisau na Gine ya Ikweta.
Jamhuri ya Gine | |
---|---|
République de Guinée (Kifaransa) Hawtaandi Gine (Kipular) ߖߌ߬ߣߍ߫ ߞߊ ߝߊߛߏߖߊߡߊߣߊ (Kimaninka) | |
Kaulimbiu ya taifa: Travail, Justice, Solidarité (Kifaransa) "Kazi, Haki, Mshikamano" | |
Wimbo wa taifa: Liberté (Kifaransa) "Uhuru" | |
Mahali pa Guinea | |
Ramani ya Guinea | |
Mji mkuu na mkubwa nchini | Conakry |
Lugha rasmi | Kifaransa |
Imepakana na Gine-Bisau, Senegal na Mali upande wa kaskazini, Kodivaa, Liberia na Sierra Leone kusini halafu Bahari ya Atlantiki upande wa magharibi.
Eneo lake ni chanzo ya mito mikubwa ya Niger, Senegal na Gambia.
Jina la "Gine" liliwahi kutaja sehemu kubwa ya Afrika ya Magharibi kati ya jangwa la Sahara na Ghuba ya Gine ya Atlantiki likimaanisha "nchi ya watu weusi" kwa lugha ya Kiberberi.
Makabila yaliyopo nchini ni 24. Kubwa zaidi ni lile la Wafulani (40%).
Lugha rasmi ni Kifaransa, lakini wakazi wanatumia zaidi lugha asilia kadiri ya makabila, hasa Kipular, Kimaninka, Kisusu, Kikisi, Kikpelle na Kiloma,
Upande wa dini, 85% ni Waislamu (hasa Wasuni), 8% ni Wakristo (hasa Wakatoliki) na 7% ni wafuasi wa dini asilia za Kiafrika.
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Guinea kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.