Bulgaria (kwa Kibulgaria: България; jina rasmi ni Jamhuri ya Bulgaria) ni nchi ya Ulaya kusini - magharibi kwenye rasi ya Balkani.

Ukweli wa haraka
Република България
Republika Balgaria

Jamhuri ya Bulgaria
Thumb Thumb
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Съединението прави силата
("Umoja huleta nguvu)
Wimbo wa taifa: Mila Rodino
("Taifa la kupendwa")
Thumb
Mji mkuu  Sofia
42°41 N 23°19 E
Mji mkubwa nchini Sofia
Lugha rasmi Kibulgaria
Serikali
Rais
Waziri Mkuu
Demokrasia
Rumen Radev (Румен Радев)
Kiril Petkov (Кирил Петков)
Uhuru
ilianzishwa
Bulgaria kuwa nchi ya kikristo
madaraka ya kujitawala
Ilitangazwa


681
865
3 Machi 1878
5 Oktoba 1908
(22 Septemba
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
110,994 km² (ya 106)
2.16%
Idadi ya watu
 - 2021 kadirio
 - 2014 sensa
 - Msongamano wa watu
 
7,000,039 (ya 106)
6,875,040[1]
63/km² (ya 118)
Fedha Lev (BGN)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
EET (UTC+2)
EEST (UTC+3)
Intaneti TLD .bg
Kodi ya simu +359

-

Funga


Imepakana na Bahari Nyeusi, Serbia, Makedonia Kaskazini na Ugiriki.

Ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya.

Historia

Zamadamu walikuweko walau miaka milioni 1.4 iliyopita.

Kufikia mwaka 5000 hivi KK kulikuwa na ustaarabu mkubwa uliotengeneza vyombo vya ufinyanzi na usonara vilivyo kati ya vile vya awali zaidi duniani.

Baada ya mwaka 3000 KK, Wathraki walijitokeza katika rasi ya Balkani.

Mwishoni mwa karne ya 6 KK sehemu kubwa ya eneo hilo lilitekwa na Dola la Persia.

Katika miaka ya 470 KK, Wathraki waliunda ufalme wa Odrusia, ambao baadaye ulianguka na wenyewe walitawaliwa na Wamakedonia, Wakelti na Warumi. Mchanganyiko huo wa watu ulikuja kuungana na Waslavi, waliolowea rasi kwa namna ya kudumu baada ya mwaka 500 BK.

Mwaka 632 Wabulgaria walianzisha nchi huru kaskazini kwa Bahari Nyeusi iliyoitwa Bulgaria Kuu chini ya Kubrat hadi nusu ya pili ya karne ya 7.

Asparukh, mwandamizi wake, alihamia karibu na delta ya mto Danube akazidi kuteka maeneo ya Balkani yaliyokuwa ya Dola la Bisanti, jambo lililoendelea katika karne zilizofuata.

Huo mchanganyiko mkubwa wa watu ulipata utambulisho wa kitaifa kwa kushika dini, lugha na alfabeti moja.

Katika karne ya 11 hilo dola la Bulgaria la kwanza lilishindwa na Dola la Roma Mashariki likisaidiwa na Warusi.

Lakini mwaka 1185 ndugu Asen na Peter walifaulu kuanzisha dola la pili la Bulgaria lililofikia kilele chake katika miaka ya 1230.

Baada ya kugawanyika, falme tatu za Kibulgaria zilitekwa na Dola la Osmani mwaka 1396 kwa miaka 500 iliyofuata.

Vita kati ya Urusi na Uturuki vya miaka 1877–1878 vilileta uhuru kwa sehemu ndogo ya Bulgaria. Kwa kutaka Wabulgaria wote wawe ndani yake, nchi iliunga mkono Ujerumani katika vita vikuu vyote viwili na hatimaye ilishindwa.

Hivyo Bulgaria ikawa chini ya Wakomunisti kwa miaka 45.

Baada ya hapo Bulgaria ilijiunga na NATO mwaka 2004 na Umoja wa Ulaya mwaka 2007.

Watu

Wakazi wanazidi kupungua tangu mwanzo wa miaka ya 1990.

Wengi wao (84.8%) wanazungumza Kibulgaria, ambacho ni kati ya lugha za Kislavoni, na wanafuata dini ya Ukristo katika Kanisa la kitaifa ambalo ni kati ya Makanisa ya Kiorthodoksi.

Pia kuna makundi makubwamakubwa ya Waturuki (8.8%) Waislamu na walowezi kutoka India (4.9%).

Kwa jumla, Wakristo ni 75%, Waislamu 10%, wenye dini nyingine ni 3%, wakati wasio na dini ni 11.8%.

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya Nje

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.