Ufinyanzi ni teknolojia na ufundi wa kutengeneza vyombo kwa matumizi ya binadamu kwa kutumia udongo wa mfinyanzi au kauri.
Udongo wa ufinyanzi unapewa umbo unaotakiwa, kukaushwa, kupambwa na kuchomwa kwa moto na kwa njia hii vyombo vigumu vinatokea kwa matumizi yanayotakiwa kama vile sahani, bakuli, chungu, kikombe au birika.
Udongo unaofaa
Udongo wa aina ya ufinyanzi ni udongo wa pekee ambao una chembechembe ndogo sana. Chembe zake ni ndogo kuliko mikromita 2. Unapokea maji na kuyashika ndani yake na katika hali ya unyevu ni laini sana una tabia ya kushikamana. Tabia hii inamruhusu mfinyanzi kuupa maumbo mbalimbali.
Lakini baada ya kukauka unakuwa mgumu. Ukichomwa motoni ugumu unaongezeka pia uwezo wake wa kuvumilia kanieneo.
Mbinu za kufinyanga udongo
Kuna mbinu mbalimbali za kufinyanga vyombo.
- vipande bapa vya udongo wa mfinyazi vinatandikwa kwa umbo kama chapati, kukatwa na kuunganishwa katika hali bichi halafu kusawazishwa.
- koili ambazo ni vipande virefu vyembamba vinabingirishwa na kupewa umbo kama kamba halafu kuviringishwa rusu juu ya rusu, halafu uso unasawazishwa.
- wafinyanzi wengi hutumia gurudumu la mfinyanzi. Kipande cha udongo wa mfinyanzi kinaviringishwa na gurudumu halafu uwazi wa ndani unatengenezwa kwa mkono au kifaa chenye umbo na umbo la nje vilevile.
- leo hii vyombo vingi vya kufinyangwa vinatengenezwa viwadani wa kutumia mashine na kalibu.
- Koili inaandaliwa
- Koili inawekwa juu ya chanzo cha chombo
- Koili ya juu inasawazishwa na kukandamizwa
Kukausha vyombo
Kupamba vyombo
Kutia kioo
Kuchoma
Historia
Viungo vya nje
Wikiwand in your browser!
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.