Vita ya Miaka Saba ilitokea kati ya miaka 1756 na 1763. Ilitokana na mashindano ya nchi za Ulaya ikasambaa pande nyingi za dunia. Hivyo imeitwa "Vita Kuu ya Dunia" ya kwanza hata kama jina hilo kwa kawaida linatumiwa kwa ajili ya vita kati ya 1914 na 1918.
Washiriki katika vita hii walikuwa nchi za Ulaya na makoloni yao, pia watu wa sehemu mbalimbali za dunia walioshikamana nao.
Katika Afrika Waingereza walitwaa kituo cha St. Louis katika Senegal kutoka Ufaransa (ilirudishwa baada ya vita)
Prussia iliweza kutetea jimbo la Silesia dhidi ya Austria ikapata sifa nyingi kwa sababu jeshi lake lilishindana na Waaustria, Warusi na Wafaransa kwa wakati mmoja. Lakini mnamo mwaka 1762 nguvu za Prussia zilikwisha ikaelekea kushindwa. Iliokolewa kwa sababu malkiaElizabeti wa Urusi alifariki na mfalme mpya Petro III alimpenda sana mfalme wa Prussia akaamua kupatana naye badala ya kumshambulia tena. Hivyo Austria ilibaki adui pekee ikashindwa.
Matokeo makuu ya vita
Uingereza ilipata kuwa nchi yenye makoloni mengi zaidi duniani baada ya Hispania ikaelekea kuipiku. Pia ilitawala bahari za dunia kwa kuwa taifa lenye manowari mengi na vituo pamoja na bandari kwenye mabara yote.
Uwezo wa Ufaransa ulipunguzwa ikipotewa na makoloni yake katika Amerika ya Kaskazini na kubaki na maeneo madogo tu katika Karibi na Uhindi.
Prussia ilitoka vitani kama nchi muhimu ya tano ya Ulaya pamoja na Ufaransa, Austria, Uingereza, na Urusi.
Matokeo ya baadaye
Msingi wa Kiingereza kuwa lugha ya kwanza duniani uliwekwa kwa sababu kilitumiwa kote katika makoloni ya Uingereza
Ushindi wa Uingereza ulikuwa msingi wa mapinduzi na uhuru wa Marekani miaka 13 baadaye. Walowezi walijifunza mitindo ya vita waliposhiriki katika vita upande wa Uingereza na walitumia ujuzi huo baadaye dhidi ya Uingereza. Kuondolewa kwa Ufaransa kulipunguza vizuizi dhidi ya upanuzi wa Marekani katika Amerika ya Kaskazini.
Uadui wa Ufaransa dhidi ya Uingereza ulibaki ukaimarishwa na kusababisha usaidizi wa Ufaransa kwa waasi wa Amerika ya Kaskazini mwaka 1776 hadi kuzaliwa kwa taifa jipya la Marekani.
Kudhoofishwa kwa Ufaransa kwa sababu ya gharama kubwa ya vita hivyo na ile ya kusaidia Wamarekani baadaye ambayo iliathiri uchumi na sifa za utawala wa kifalme na kuwa sababu muhimu ya mapinduzi ya Kifaransa
Ushindi wa Prussia ulisababisha mashindano ya mfululizo kati ya Prussia na Austria juu ya kipaumbele katika Ujerumani yaliyoonekana baadaye hadi vita ya 1866.
Friedrich II wa Prussia
George II wa Hannover na Uingereza
Maria Theresia wa Austria
Louis XV wa Ufaransa
Elisabeth wa Urusi (hadi 1762)
Peter III wa Urusi (tangu 1762)
Adolf Fredrik wa Uswidi
"Mjane wa mwanajeshi aombaomba" - tokeo la vita lilikuwa umaskini kwa watu wengi
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Vita ya Miaka Saba kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Wikiwand in your browser!
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.