From Wikipedia, the free encyclopedia
Elizabeti wa Urusi (kwa Kirusi Елизавета Фёдоровна Романова, Elizabeth Feodorovna Romanova; 1 Novemba 1864 – 18 Julai 1918) alikuwa mwanamke wa ukoo tawala wa jimbo mojawapo la Ujerumani aliyeolewa na mtoto wa tano wa kaisari Alexander II wa Russia.
Baada ya mumewe kuuawa kwa bomu mwaka 1905, Elisabeti alimsamehe muuaji, Ivan Kalyayev, na kujitahidi asiadhibiwe.
Kisha kuhama ikulu, akawa mmonaki akaanzisha konventi ya Marfo-Mariinsky ili kusaidia pia maskini wa Moscow.
Mwaka 1918 alikamatwa na kuuawa na Wakomunisti.
Elizabeti alitagazwa na Waorthodoksi kuwa mtakatifu mwaka 1981 na mwaka 1992.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.