From Wikipedia, the free encyclopedia
Vita vya Ufaransa na Waindio vilikuwa vita vya kimataifa kutoka mwaka wa 1754 hadi mwaka wa 1763. Vita vilitokea baada ya miaka mingi ya mapigano kati ya Uingereza, Hispania, na Ufaransa katika maeneo ya kikoloni ya Amerika Kaskazini. Waindio waliingia vitani pande zote mbili, kadiri ya makabila yao.
Vita hivyo vinatazamwa kwa kawaida kama sehemu ya Vita vya Miaka Saba vilivyoenea katika kontinenti tano miaka 1756-1763.
Miaka ya 1700, mamlaka ya kikoloni katika Amerika Kaskazini yalikuwa yakipanuka haraka. Kwa sababu hiyo, maeneo mengi ya kikoloni yalianza kugongana. Katika mwaka wa 1756, Uingereza ilitangaza vita dhidi ya Ufaransa, tukio ambalo Winston Churchill alisema kuwa lilianza “vita vya kwanza vya dunia”, kwa sababu vita hivyo vilihusisha nchi nyingine duniani kote.[1] Uingereza na Ufaransa walikuwa viongozi muhimu wa vita hivyo. Vita kati ya Uingereza na Ufaransa vilianzia Pennsylvania katika mwaka wa 1754.
Chanzo kikuu cha Vita vya Ufaransa na Waindio kilikuwa upanuzi wa eneo la Kifaransa katika bonde la Mto Ohio. Eneo hilo, ambalo sasa ni jimbo la Pennsylvania, lilipakana na makoloni ya Uingereza kwenye pwani ya mashariki ya Marekani ya leo. Katika mwaka wa 1754, Wafaransa walijenga Ngome ya Duquesne mahali ambapo Mto Allegheny na Mto Monongahela hukutana, ambapo ni Pittsburgh sasa. Mahali hapo palikuwa muhimu kwa sababu palidhibiti matumizi ya Mto Ohio. Waingereza walianza kushambulia Ngome ya Duquesne katika mwaka wa 1754.[2]
Katika miaka michache ya kwanza, Waingereza walijitahidi. Ufaransa na washirika wa Waindio walijua jiografia ya eneo hilo na walikuwa na msaada kutoka kwa wenyeji. Katika mwaka wa 1757, vita vilianza kubadilika. [Pitt, 1st Earl of Chatham|William Pitt] alifanywa kuwa waziri mkuu mpya wa Uingereza na alijua kwamba kuujenga ufalme mkubwa wa Uingereza kulihitaji kudhibiti makoloni ya Amerika. Serikali ya Uingereza iliulipa ufalme wa Prussia kupigana vita Ulaya na Uingereza waliwatuma askari zaidi katika vita Amerika.
Mnamo Julai 1758, Uingereza walishinda vita vikubwa katika Louisburg juu ya Mto Saint Lawrence. Udhibiti wa mto huo uliwatia mashakani wanajeshi wa Ufaransa katika Kanada. Katika mwaka wa 1758 pia, jeshi la Uingereza liliikamata Ngome ya Duquesne na kuibadili jina kuiita Ngome ya Pitt. Katika kipindi cha miaka miwili iliofuata, jeshi la Uingereza lilishambulia maeneo mengine ya Kanada yaliyomilikiwa na Ufaransa. Mnamo Septemba 1759, askari wa Uingereza wakiongozwa na Jenerali James Wolfe walishambulia Jiji la Quebec.[3] Mashindano hayo yalikuwa sehemu muhimu ya vita. Uingereza walishinda mashindano ya Quebec na baadaye mwaka huo waliteka Montreal, mji wa mwisho wa Ufaransa nchini Kanada.
Kwa miaka mitatu iliyofuata, vita vilipiganwa katika sehemu nyingine za dunia kama Ulaya. Uingereza walikuwa wameshinda Ufaransa katika Amerika Kaskazini.
Katika mwaka wa 1763, vita vilikwisha na Mkataba wa Paris.[4] Uingereza walipokezwa makoloni ya Ufaransa huko Amerika na Florida kutoka Hispania. Huo ulikuwa mwisho wa utawala wa Ufaransa huko.
Serikali ya Ufaransa ilibaki na madeni mengi na hayo yalichangia sana Mapinduzi ya Ufaransa miaka ishirini baadaye. Mapinduzi hayo tena yalileta athari nyingi sana.
Kwa Uingereza, vita vilikuwa vya mafanikio na vilifanya makoloni Marekani thabiti. Kwa bahati mbaya kwa Uingereza, vita vilikuwa ghali sana kwao pia na kuwasukuma katika madeni. Vita ya uhuru wa Marekani miaka kumi na mmoja baadaye vilisababishwa na kodi ambazo ziliwekwa kwa watu wa Marekani. Uamuzi wa Ufaransa kusaidia Marekani katika vita hivyo ulisababishwa na chuki dhidi ya Uingereza kwa sababu ya kupoteza vita dhidi ya Waindio. Walowezi walijifunza mitindo ya vita walipovishiriki upande wa Uingereza wakatumia ujuzi huo baadaye dhidi ya Uingereza. Kuondolewa kwa Ufaransa kulipunguza vizuizi dhidi ya upanuzi wa Marekani katika Amerika ya Kaskazini.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.